Nav bar

Jumatatu, 23 Juni 2025

MILIONI 268 ZATUMIKA UKARABATI MNADA WA KINTINKU MANYONI

Na. Hamis Hussein

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekamilisha kwa asilimia 100 ujenzi wa uzio wenye mzunguko wa mita za mraba 500 katika Mnada wa Kinyinku wilayani Manyoni wenye thamani ya shilingi milioni 268, fedha zilizotengwa katika bajeti ya mwaka 2022/ 2023 ikiwa ni sehemu ya ukarabati wa miundombinu kwa ajili ya mazingira wezeshi ya biashara ya mifugo na mazao yake nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti leo Juni 23, Mwaka 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Manyoni Mashariki Mhe. Dkt. Pius Chaya, lililohoji ni  lini  serikali itakamilisha ujenzi wa uzio wa mnada wa Kintinku uliopo Halmashauri  ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Aidha Mhe. Mnyeti ameongeza kuwa  serikali itaendelea kuboresha mindombinu muhimu kurahisisha biashara hiyo katika maeneo mbalimbali nchini.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni