Nav bar

Jumamosi, 25 Oktoba 2014

SHAMBA LA KUTOTOLESHA VIFARANGA VYA SAMAKI NA WATENGENEZAJI WA CHAKULA CHA SAMAKI EDEN AGRI-AQUA LTD PUGU KINYAMWEZI DAR-ES-SALAAM TANZANIA


Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt Titus Kamani mara baada ya kuwasili katika shamba la Eden Agri-Aqua LTD na kupokelewa na mwenyeji wake Bw William Bwemelo katika eneo la Pugu Kinyamwezi nje kidogo ya Jiji la Dar-es-salaam
Waziri Kmani akaribishwa katika Ukumbi wa Mkutano wa shamba la Eden Agri-Aqua LTD
Katibu wa Waziri Bw Eliukana  Mwakipesile, akifatilia jambo wakati wa maelezo ya Mmiliki wa shamba la Eden kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt Titus Kamani hayupo pichani


 Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt Titus Kamani akiangalia utotoleshaji wa vifaranga vya samaki aina ya perege kwenye shamba la Eden Agri-Aqua LTD lililopo nje kidogo mwa Jiji la Dar-es-salam Pugu KinyamweziMmiliki wa shamba la Eden Bw William Bwemelo akimuonyesha Waziri Kamani Mtungo wa hewa ya Oxygen inayotumika kuweka kwenye vyombo vya kusafirishia vifaranga vya samaki wateja wanaponunua
Meneja wa shamba la uzalishaji vifaranga akitoa maelezo kwa Mhe Waziri Kamani
Hali ya hewa imebadilika ghafla mvua imeanza kunyeshaMeneja wa shamba aliendelea kutoa maelezo ya uzalishaji na utunzaji wa vifaranga vya samaki kwa Mhe. Waziri Kamani


Mhe Dkt Titus Kamani Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi alishuhudia mabwawa ya aina mbalimbali ya kulelea samaki wazazi , wakuuzwa kwa ajili ya chakula , wadogo na vifaranga vinavyouzwa kwa wateja wanaohitaji hapa Tanzania
Mhe Waziri alipata nafasi ya kuwapa samaki chakula na kuona jinsi chakula kinachokubalika kinachoelea kinavyoweza kuliwa na samaki hao
Mhe Waziri alipata nafasi ya kuwapa samaki chakula na kuona jinsi chakula kinachokubalika kinachoelea kinavyoweza kuliwa na samaki hao


Eneo linalotumika kukuzia vifaranga vya samaki mara wanapotoka kwenye mashine za kutotolesha

Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt Titus Kamani akielekea kwenye Jengo linalotumika kwa uzalishaji wa chakula cha samaki ambapo mashine mbalimbali za kuandaa chakula hicho zimefungwa
Hiki ndio chakula cha samaki kilichohakikiwa na wataalam wa samaki, mchanganyiko wake ni bara kwa makuzi ya samaki au viumbe kwenye maji
Meneja uzalishaji wa vyakula vya samaki akitoa maelezo kwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugio na Uvuvi Mhe. Dkt Titus Kamani juu ya utengenezaji wa vyakula hivyo
Waziri Kamani aliuliza maswala kadhaa ya kutaka uhakika wa ubora wa chakula hicho kuanzia mwanzo hadi mwisho

Mhe Dkt Titus Kamani, akikagua chakula malighafi zinazotengeneza mchanganyiko wa chakula cha samaki pembeni ni Mmiliki wa Eden Agri-Aqua akimtazama malighafi hiyo

Bw William Bwemelo akitoa maelezo kwa Waziri Kamani

Mhe Dkt Kamani akiangalia moja ya mashine zinazo tengeneza aina ya chakula cha samaki chenye uwezo wa kuelea juu ya maji, ambacho ndicho kinachopendekezwa na wataalam wa Ufugaji Viumbe kwenye Maji
Mhe Wziri akiangalia kifungashio cha chakula hicho cha samaki
Bi Eva Sessoa kutoka TBC-1 akichukua picha za luninga tayari kwa kuwasilisha Habari juu ya ziara ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt Titus Kamani katika shamba la Eden Agri- Aqua LTD
Mhe Waziri Kamani akishika chakula hicho kilicho katika mfumo wa pellets
Mkononi mwa Waziri ameshika chakula cha samaki na anaangalia ubora wake kwa karibu zaidi

Chakula cha samaki kilichotengenezwa kwa mfumo wa pelets kikiwa kimeanikwa kwenye mikeka maalum ili kikauke vizuri

Maoni 5 :

 1. Kifaranga cha kambare ni bei gani??

  JibuFuta
 2. Nahitaji kujua bei ya chakula cha samaki katika hiko kiroba chenye ujazo wa 25kg

  JibuFuta
 3. Naomba msaada wa namna ya kuandaa banda la kufugia samaki (sato na kambale), pia kufahamu bei ya vifaranga.

  JibuFuta
 4. Naomba msaada wa namna ya kuandaa banda la kufugia samaki (sato na kambale), pia kufahamu bei ya vifaranga.

  JibuFuta