Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe leo tarehe 19Julai,2023 jijini Dar es Salaam amekutana na Uongozi wa Shirika la Misaada la ujerumani (GIZ) na kufanya kikao na Uongozi wa GIZ Tanzania pamoja na Uongozi wa Hifadhi za Bahari na maeneo Tengefu (MPRU), TAFICO pamoja na maafisa wengine wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Lengo la Kikao hicho ni kumjulisha Katibu Mkuu kuhusu mradi wa “Transboundary conservation and sustainable management of coastal and marine biodiversity" utakaofadhiliwa na Serikali ya ujerumani kupitia shirika lake la Misaada la (GIZ) kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya.
Aidha, Mradi huo wa “Transboundary conservation and sustainable management of coastal and marine biodiversity, utatekelezwa katika maeneo ya Kwale Tanga,Tanzania,pamoja na Kenya.
Vilevile, Mradi huo utakuwa na shughuli nyingi ikiwemo uhifadhi wa mazingira, uchumi na kuongeza uwezo na maendeleo kwa jamii ya Kitanzania.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (kulia) akimsikiliza kwa Makini Bw.Jens Bruggemann,Kiongozi kutoka shirika la Misaada la Ujerumani (GIZ) katikati, akielezea namna mradi wa “Transboundary conservation and sustainable management of coastal and marine biodiversity utakavyofanya Kazi nchini Tanzania. Kushoto ni Dkt.Immaculate Sware, Meneja wa MPRU.
Picha ya Pamoja ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Shemdoe na baadhi ya Maafisa walioshiki kikao hicho leo tarebe 19/07/2023 jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakimsikiliza Bw. Jens Bruggemann,Kiongozi wa Shirika la Misaada la uzjrumani GIZ (Hayupo pichani) akieleza maeneo ambayo mradi huo utatekelezwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni