Na. Elibariki Mafole, Mpwapwa
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,
Pauline Gekul ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI)
kujiendesha kibiashara ili iweze kukabiliana na changamoto zinazo ikabili.
Gekul ameyasema hayo leo (15.03.2021)
wakati alipo tembelea kituo cha TALIRI na LITA Mpwapwa kwa lengo la kukagua
kazi zinazofanywa na taasisi hizo.
Katika taarifa iliyosomwa na Kaimu
Mkurugenzi Mkuu TALIRI, Dkt. Jonas Kizima ilielezea changamoto wanazokabiliana
nazo zikiwemo za upungufu wa watumishi, uhaba wa vitendea kazi na uhaba wa
rasilimali fedha kwa shughuli za kiutafiti. Lakini pia alizungumzia mikakati
waliyonayo katika kukabiliana na changamoto hizo.
Kwa kuwa changamoto nyingi zinahitaji
fedha ili kuzitatua ndipo Naibu Waziri Gekul akawaagiza TALIRI kujipanga vizuri
ili sasa waweze kujiendesha kibiashara kwani kwa kufanya hivyo wataweza kutatua
changamoto walizonazo badala ya kusubiri kupata fedha kutoka Serikalini.
Pia amewapa miezi mitatu kuhakikisha
wanawalipa vibarua wanaochunga ng'ombe pamoja na walinzi mishahara yao ya miezi
sita wanayodai.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Jabir
Shekimweri amemshukuru Naibu Waziri kwa maamuzi yake ya kitembelea taasisi hizo
na kutatua tatizo la mishahara ya vibarua na walinzi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TALIRI, Bw.
Jonas Kizima amesema wamepokea maelekezo yaliyotolewa na Naibu Waziri na
watakwenda kuyafanyia kazi hasa suala la taasisi hiyo kujiendesha kibiashara.
Katika ziara yake hiyo Wilayani Mpwapwa, pia ametembelea wilaya ya Kongwa ambapo amatembelea Ranchi ya Kongwa, shamba la malisho la mfugaji Bw. Mnyonaki lililopo katika kijiji cha Msunjilile wilayani Kongwa na Machinjio ya kuku iliyopo katika kijiji cha Mbande wilayani Kongwa.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na Viongozi na watumishi wa TALIRI na LITA Mwapwapwa pamoja na viongozi wa Wilaya wakati alipotembelea taasisi hizo kwa lengo la kukagua shughuli zinazofanyika. (15.03.2021)Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na wachungaji wa ng'ombe (waliosimama
kushoto) wanaomilikiwa na taasisi ya TALIRI Mpwapwa wakati alipotembelea
taasisi ya TALIRI na LITA Mpwapwa kwa lengo la kukagua shughuli zinazofanyika.
Waliosimama kulia ni Viongozi kutoka Wizarani, TALIRI, LITA na Viongozi wa
Wilaya ya Mpwapwa. (15.03.2021)
Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi
ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa kabla ya kuanza ziara yake ya kikazi wilayani
humo.(15.03.2021)
Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na Viongozi wa NARCO na baadhi ya
viongozi wa Wilaya ya Kongwa wakati alipotembelea Ranchi ya Kongwa kwa lengo la
kukagua shughuli zinazofanyika. (15.03.2021)
Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na Mama Salma Kikwete (wa kwanza kulia)
katika duka la nyama kwenye Ranchi ya Kongwa wakati alipotembelea Ranchi hiyo
kukagua shughuli zinazofanyika. (15.03.2021)
Naibu Waziri wa Mifugo na
Uvuvi, Mhe. Pauline Gekul akizungumza na Bw. Mnyonaki (wa kwanza kushoto)
ambaye ni mfugaji na mkulima wa malisho ya Mifugo katika kijiji cha Msunjilile
Wilayani Kongwa wakati alipomtembelea kwa lengo la kuona shamba lake la malisho.
(15.03.2021)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni