Kaimu Muhifadhi Mfawidhi,
Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Bw. Amin Abdallah (kushoto) akisoma
taarifa ya utekelezaji wa Majukumu ya taasisi hiyo kwa Makatibu Wakuu kutoka
Wizara nne tofauti walipotembelea taasisi hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah. (22.08.2020)
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (kulia) akieleza jambo kwa Mkuu wa
Wilaya ya Mafia, Bw. Shaib Nnunduma (kushoto) wakati wa kikao cha Makatibu
Wakuu na Mkuu huyo wa Wilaya pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama ya
Wilaya kilichofanyika katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya. (22.08.2020)
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (Kulia) akiongea na Watumishi wa
Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) (hawapo pichani) alipotembelea
Taasisi hiyo iliyopo katika eneo la Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa cha Mafia.
Kushoto ni Kaimu Muhifadhi Mfawidhi, Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU),
Amin Abdallah. (22.08.2020)
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (Kulia) akiongea na Watumishi wa
Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) (hawapo pichani) alipotembelea
Taasisi hiyo iliyopo katika eneo la Hifadhi ya Bahari ya Kisiwa cha Mafia.
Kushoto ni Kaimu Muhifadhi Mfawidhi, Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU),
Amin Abdallah. (22.08.2020)
Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Bw.
Shaib Nnunduma (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu
walipotembelea Ofisi yake. Kutoka kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa
Rais, Muungano na Mazingira, Injinia Joseph Malongo, wa pili kulia ni Katibu
Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah. Wa kwanza
kushoto ni Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Gerald Mweli na wa pili kushoto ni
Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Alloyce Nzuki. Wengine pichani ni
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Kisiwani Mafia.
Mhifadhi Mshirikishi Jamii,
Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU), Albert Makala (katikati) akieleza
jambo mbele ya Makatibu Wakuu katika kikao kilichofanyika kwenye Ofisi za MPRU
zilizopo Kisiwani Mafia. Kulia anayemuangalia ni Katibu Mkuu, Wizara ya
Maliasili na Utalii, Bw. Alloyce Nzuki. Wengine pichani ni Watumishi wa MPRU. (22.08.2020)
Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo
na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (wa pili kutoka kulia waliosimama
mbele) akiwa na Makatibu wa Wakuu wenzake, kutoka kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi
ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Injinia Joseph Malongo. Kushoto ni
Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Bw. Gerald Mweli na wa pili kushoto ni Katibu
Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw. Alloyce Nzuki wakiwa katika picha ya
pamoja na Watumishi wa Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) walipotembelea
ofisi za MPRU. (22.08.2020).
Makatibu wa Wakuu kutoka
Wizara nne tofauti wakimsikiliza Mwenyekiti wa Wavuvi wanaoishi katika Kisiwa
cha Nyororo kilichopo katika Kisiwa cha Mafia, Bw. Likua Said Mchomoko (kulia
aliyevaa Tshirt ya Njano) alipokuwa akitoa maelezo kuhusu shughuli za uvuvi
wanazozifanya katika eneo hilo. Wa kwanza kutoka kulia waliosimama ni Katibu
Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Injinia Joseph Malongo na
wa pili kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, anayesimamia Elimu, Bw.
Gerald Mweli. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Bw.
Alloyce Nzuki na wa pili kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na
Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah. (23.08.2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni