Naibu Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akikagua ramani ya ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za
ngozi Kilimanjaro Leather Industries Co. Ltd kilichopo katika eneo la Gereza la
Karanga Mkoani Kilimanjaro, ambapo ujenzi wa kiwanda hicho utagharimu zaidi ya
Shilingi Bilioni 60. Pembeni yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho
Mhandisi Masoud Omary. (08.08.2020)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah
Ulega akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika katika ofisi za Mkuu wa
Mkoa wa Kilimanjaro akiwa na baadhi ya maafisa kutoka katika wizara hiyo na
kukutana na mkuu wa mkoa huo Dkt. Anna Mghwira ambapo wamezungumza mambo
mbalimbali ya kuboresha sekta ya mifugo na uvuvi kabla ya kuelekea katika
Gereza la Karanga kujionea ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha
Kilimanjaro Leather Industries Co. Ltd. (08.08.2020)
Naibu Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akikagua baadhi ya mitambo itakayofungwa katika
kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro Leather Industries Co. Ltd kilichopo
katika eneo la Gereza la Karanga Mkoani Kilimanjaro na kusisitiza watanzania
kununua bidhaa za ngozi zinazozalishwa hapa nchini ili kuunga mkono jitihada
zinazofanywa na wawekezaji pamoja na wajasiriamali. (08.08.2020)
Muonekano wa maendeleo
ya ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Kilimanjaro Leather Industries Co.
Ltd kilichopo katika Gereza la Karanga Mkoani Kilimanjaro, ambapo Naibu Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amelipongeza Jeshi la Magereza Mkoa wa
Kilimanjaro kwa kutumia nguvu kazi ya wafungwa kwa ajili ya ujenzi huo ambapo
baadhi ya wafungwa wamepatiwa pia elimu ya ujenzi katika gereza hilo.
(08.08.2020)
Naibu Waziri wa Mifugo
na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akikagua ubora wa matofali yanayotengenezwa na
wafungwa wa Gereza la Karanga kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za
ngozi cha Kilimanjaro Leather Industries Co. Ltd kilichopo katika eneo la
gereza hilo, ambapo ameridhishwa na ubora wa matofali hayo ambayo ni
mchanganyiko wa saruji na vumbi la miamba/mawe. (08.08.2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni