Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya ndani, Mhe.
George Simbachawene akiangalia mbegu bora za malisho ya wanyama zinazozalishwa
na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo(TARILI) alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo
na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye Viwanja vya Nzuguni,
Kanda ya Kati, Dodoma Agosti 7, 2020.
Afisa Mauzo, Kampuni
ya Inas, Hussein Juma(kulia) akimkaribisha Mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya
Ndani, Mhe. George Simbachawene kuonja vipande vya Nyama
vilivyokaushwa na kutafunwa kama kichangamsha mdomo alipotembelea banda la
Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye
Viwanja vya Nzuguni, Kanda ya Kati, Dodoma Agosti 7, 2020.
Mkuu wa Kitengo cha
Uhimilishaji, Kanda ya Kati, Idara ya Uzalishaji na Masoko, Denis
Sichwale(Kulia) akitoa maelezo kuhusu Uhimilishaji kwa Mgeni rasmi, Waziri wa
Mambo ya Ndani, Mhe. George Simbachawene alipotembelea banda la Wizara ya
Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea kwenye Viwanja vya
Nzuguni, Kanda ya Kati, Dodoma Agosti 7, 2020.
Mratibu wa Maonesho, banda la Wizara ya Mifugo
na Uvuvi, Bezia Rwongezibwa (wa pili kulia) akimkaribisha Mgeni rasmi, Waziri
wa Mambo ya Ndani, Mhe. George Simbachawene (kushoto, aliyevaa kaunda suti)
alipotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Maonesho ya Nane Nane
yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni, Kanda ya Kati, Dodoma leo Agosti 7,
2020.
ARUSHA
Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro Dkt. Anna Mgwira akipata maelezo ya ufugaji wa sungura kutoka
kwa mtaalam wa sungura wa kampuni ya SAORE, Bw. Isack John kwenye maonyesho ya
nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha.
(07/08/2020)
Mkufunzi kutoka
Wakala ya vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA), Bw. Ijumaa Bakari akitoa maelezo
kwa wadau waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya
nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha.
(07/08/2020)
Msambazaji wa madini
ya Mifugo kutoka kampuni ya usambazaji wa madini (JOSERA), Bw. Elirehema
Laizer akitoa elimu ya madini na umuhimu wake kwa Mifugo kwa wadau
waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane
yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi Mkoani Arusha. (07/08/2020)
Daktari wa Mifugo
kutoka kituo cha Uhimilishaji NAIC, Bw. Elibariki Njiku akitoa elimu kwa
wanafunzi wa shule ya msingi Suye waliotembelea banda la Wizara ya Mifugo na
Uvuvi kwenye maonyesho ya nanenane yanayoendelea kwenye kiwanja cha Themi
Mkoani Arusha. (07/08/2020)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni