Timu ya soka kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetinga hatua ya robo fainali ya michuno ya SHIMIWI 2023 inayoendelea mkoani Iringa baada ya kuishindilia timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani goli 1-0 leo Oktoba 06, 2023 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Samora.
Goli hilo limefungwa na mshambuliaji hatari wa timu hiyo Joseph Buhigwe dakika ya 35 ya mchezo baada ya vuta nikuvute iliyotokea kwenye lango la timu ya timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani kabla ya mpira kufika kwa Buhigwe aliyeachia shuti kali lililozama wavuni moja kwa moja.
Timu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilionekana kuutawala mchezo huo wakati wote na kama si uimara wa mabeki na golikipa wa timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani huenda wangefungwa magoli mengi zaidi.
Baada ya ushindi huo Wizara ya Mifugo na Uvuvi sasa imeingiza timu 2 kwenye hatua ya robo fainali baada ya kutanguliwa na timu ya kamba wanaume waliofuzu hatua hiyo mapema leo asubuhi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni