Timu ya Mpira wa pete kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendeleza wimbi lake la ushindi kwenye michuano ya SHIMIWI baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida kwa jumla ya magoli 25-11 mchezo uliochezwa leo Oktoba 03, 2023 kwenye uwanja wa RUCU B mkoani Iringa.
Kwa ushindi huo timu hiyo imezidi kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutinga hatua ya 16 bora ambapo sasa italazimika kusubiri kukamilika kwa michezo mingine hatua ya makundi ili kubaini timu zilizofuzu hatua hiyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni