◾ Yatinga nusu fainali mita 100 na 200.
Mkimbiaji Deonatus Magendelo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi amefanikiwa kushika nafasi ya 3 kwenye mashindano ya riadha umbali wa mita 3000 mbio zilizofanyika kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa leo Oktoba 05, 2025.
Magendelo amefanikiwa kushika nafasi hiyo mara baada ya kuwapiku wanariadha wenzake 54 waliokuwa nyuma yake ambao kwa muda mrefu walionekana kuwa na ushindani wakati wote wa mbio hizo.
Kwa upande wa wanawake umbali huo huo mkimbiaji Beatrice Ilomo kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi licha ya kushindwa kushika nafasi za juu amefanikiwa kumaliza mbio hizo jambo ambalo limewashinda baadhi ya wanariadha wenzake.
Katika hatua nyingine Mwanariadha Fihiri Mbawala amefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya mbio za mita 200 mara baada ya kufanikiwa kushika nafasi ya 2 kwenye kundi lake.
Kwa upande wa mbio za mita 100 wakimbiaji William Valentino na Nuru Musa nao wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya mbio hizo ambapo William Valentino amefuzu hatua hiyo baada ya kukamilisha raundi ya kwanza akiwa kinara wa kundi lake huku Nuru Musa akishika nafasi ya 3 kwenye kundi lake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni