Nav bar

Jumatatu, 9 Oktoba 2023

KAMBA WANAWAKE WAFUZU 16 BORA

Ni baada ya kuwagaragaza RAS Kilimanjaro 


Timu ya kamba upande wa wanawake kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya SHIMIWI inayoendelea mkoani Iringa baada ya kushinda mvuto 1-0 dhidi ya timu ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro leo Oktoba 03, 2023 mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Mkwawa.


Timu hiyo iliibuka na ushindi huo kwenye raundi ya pili ya mchezo huo ambapo raundi ya kwanza iliisha kwa timu hizo kutoshana nguvu.


Timu hiyo inakuwa ya pili kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kufuzu hatua hiyo ikitanguliwa na ile ya Kamba wanaume ambayo ilifuzu mara baada ya mechi zake tatu za awali.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni