Wataalam na
wadau wa sekta ya Mifugo Nchini,
wamekutana jijini Arusha kwa lengo la kujadili namna ya kuongeza
uzalishaji katika sekta hizo ambayo italeta tija kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa chama cha wataalamu wazalishaji
mifugo na Uvuvi ,Dkt. Jonas Kizima katika ziara ya kutembelea mbuga
ya Tarangire, ikiwa ni sehemu ya kongamano la siku tatu la kisayansi
liloanza Oktoba 26 jijini Arusha
Alisema kuwa lengo
kubwa ni kupitia machapisho ya kisayansi yaliyoletwa na wadau ili
angalau waweze kutoa matokeo ya tafiti, na kutatua changamoto katika
sekta ya Mifugo na Uvuvi
"Katika hizi siku
tatu, tumetenga siku moja ya kuja kutembelea mbuga za wanyama nchini, na mwaka
huu tumechagua Tarangire ili kupata muda wa kufurahi na
kujifunza zaidi, Pia tunaunga juhudi za Rais katika kuongeza watalii nchini
kupitia Royal tour na kuongeza pato kupitia utali,"alisema Dkt.
Kizima
Naye Dkt Zablon Nziku,
alisema kuwa katika kongamano hilo pia wameweza kujadili kwa kina
Teknolojia bora zilizotumika au zinazotumika katika kuwasaidia wadau
wetu kuongeza uzalishaji.
"Pamoja na kujifunza
mambo mbalimbali ya kisayansi katika uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi nchini,
bado tunaona ipo haja ya kufanya ziara kwenye vivutio vyetu vya utalii
ili kuwaonyesha wageni kutoka nje, nasi tunaweza kufanya utalii, hii
itasaidia ongezeko la watali wa ndani,"alisema
Aidha baadhi ya
washiriki akiwemo Bi. Neema Urassa alisema kufanyika kwa
ziara hiyo kutawasaidia watumishi na wadau wa sekta hiyo kutambua vivutio vya
hapa nchini.
"Pia itamjengea
mtumishi anaporudi katika eneo lake la kazi kufanya kazi kwa jitihada na
inaongeza ufanisi wa kazi, kwa kufanya hivi kwa sekta zote kutaongeza utalii wa
ndani na kuongeza pato la nchi,"alisema Bi. Neema
Sehemu ya wataalam wazalishaji mifugo na Uvuvi wakiwa kwenye picha za pamoja katika ziara ya kutembelea mbuga ya Tarangire, ikiwa ni sehemu ya kongamano la siku tatu la kisayansi liloanza Oktoba 26 jijini Arusha
Sehemu ya wataalam wazalishaji mifugo na Uvuvi wakiwa kwenye picha za pamoja katika ziara ya kutembelea mbuga ya Tarangire, ikiwa ni sehemu ya kongamano la siku tatu la kisayansi liloanza Oktoba 26 jijini ArushaSehemu ya wanyama wanaopatikana kwenye mbuga ya Tarangire.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni