Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia mshiriki wake Siraji Mohammed imefanikiwa kushika nafasi ya 3 kwenye mashindano ya mbio za baiskeli umbali wa Km.40 yaliyofanyika leo Oktoba 08, 2023 kwenye michuano ya SHIMIWI inayoendelea mkoani Iringa.
Siraji ambaye alionesha upinzani wa hali ya juu na kuwa miongoni mwa washiriki 3 wa kwanza walioanza mzunguko wa pili kukamilisha umbali huo huku akitetea nafasi ya 3 aliyoibeba kwenye mashindano ya mwaka jana yaliyofanyika mkoani Tanga.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi itakuwa kibaruani tena leo mchana kwenye hatua ya robo fainali ambapo timu yake ya mpira ya miguu itapepetana na timu ya Bunge huku upande wa mchezo wa kamba wanaume watachuana vikali na timu ya Ikulu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni