Nav bar

Jumatatu, 9 Oktoba 2023

MIFUGO NA UVUVI YATINGA FAINALI RIADHA MITA 100

◾ Yafikia rekodi yake ya mwaka jana kupitia kwa mwanariadha yule yule. 


Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia kwa mwanariadha wake William Valentino imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya riadha umbali wa mita 100 baada ya kukamilisha hatua ya nusu fainali akiwa mshindi wa 2.


Kwa hatua hiyo William anaifikia rekodi aliyoiweka kwenye michuano ya SHIMIWI msimu uliopita ambapo pia alifanikiwa kutinga hatua ya fainali.


Mpaka sasa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefanikiwa kushika nafasi ya 3 kwenye riadha upande wa mita 3000, imeingia fainali upande wa mita 100 na nusu fainali upande wa mita 200.


Michuano ya SHIMIWI itaendelea tena kesho Oktoba 06, 2023  kwa hatua ya 16 bora ambapo kwa upande wa mpira wa miguu timu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi itamenyana na timu ya Mashitaka kwenye uwanja wa Samora majira ya saa 8 kamili mchana, timu ya kamba wanawake itachuana na timu ya Mahakama saa 12:30 asubuhi kwenye uwanja wa Mkwawa huku timu ya kamba wanaume ikitoana jasho na timu ya Wizara ya Afya.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni