◾ Kufutiwa kwa matokeo yake ya ushindi kwazua utata na kushangaza wengi.
Mchezaji Theodata Salema kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi amefanikiwa kuipa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ushindi wa nafasi ya 3 kwenye mchezo wa kurusha tufe uliofanyika leo Oktoba 05, 2023 uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Mchezaji huo alirusha mitupo yote mitatu na kupata ushindi wa mita 10. 05 kwenye mtupo wa kwanza na 7.45 kwenye mtupo wa pili huku mtupo wake wa 3 ukifutwa baada ya kurusha tufe nje ya mstari.
Hata hivyo katika hali iliyowashangaza wengi waliokuwa wakishuhudia mashindano hayo matokeo ya mtupo wa mita 10.5 yaliyopaswa kumpa ushindi kwenye mitupo yote mitatu ambayo yalikubaliwa hapo awali na waamuzi wote yalifutwa baadae ambapo ilibainika kuwa alilalamikiwa na mmoja wa viongozi wa timu zilizokuwa zikishiriki wakidai hakuweka mkono wake mahala sahihi wakati akirusha tufe jambo lililolalamikiwa na wengi kuwa ameonewa.
Mshindi wa kwanza katika mashindano hayo upande wa wanawake ni Tume ya walimu na wa pili ni Mawasiliano.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni