Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Kamati tendaji ya mradi wa ushirikiano kati ya Nairobi Convention na Southwest Indian Ocean Commission imekutana jijini Tanga kwa ajili ya kufanya tathmini ya mradi huo unaolenga usimamizi wa mazingira ya bahari na nchi kavu pamoja na usimamizi wa rasilimali za uvuvi
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI ), Dkt. Ismael Kimirei Oktoba 04,2023 ambapo amesema kuwa mradi huo unaotekelezwa katika Wilaya ya Mkinga na Pemba unalenga kutoa majibu ya mahitaji katika uchumi wa buluu
Tumeanzia eneo la Mkinga kwa sababu huu ni mradi wa ushirikiano kati ya Tanzania, Msumbiji na Madagascar na tunategemea kwamba utapanuka kwenda nchi nyingine na ukiangalia upande wa kaskazini mwa bahari ya Hindi kuna nchi ya Kenya ambayo tunatarajia iwe mdau katika mradi huu" amesema Bi. Oliver
Naye Mratibu wa Mradi unaoshughulikia maendeleo ya usimamizi wa rasilimali za bahari kutoka Shirika la Chakula na kilimo (FAO) Bi. Oliver Mkumbo amesema kuwa mradi huo unathamani ya dola za marekani milioni 8 ambazo zimegawanywa katika nchi tatu
"Kubwa ni kuangalia namna gani tuboreshe mazingira lakini wakati huo huo kuangalia rasilimali zilizopo ukanda wa Pwani zimekuwa endelevu na maisha ya watu yameboreshwa kwa shughuli zinazofanyika
Kwa upande wake Afisa uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Bw. Ezra Katete amesema kuwa mradi huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya kushirikishwa kulinda maeneo yao hususani katika utunzaji wa mazingira na kufanya uvuvi endelevu.
Mkurugenzi wa Taasisi ya
Utafiti wa Uvuvi Tanzania Dkt. Ismael Kimirei akiongea na wajumbe wakati wa kufungua kikao cha kamati tendaji
cha mradi wa ushirikiano wa SWIOFIC Nairobi Convention kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha VETA
Mkoani Tanga, Oktoba 04,2023.
Mratibu wa Mradi
unaoshughulikia maendeleo ya usimamizi wa rasilimali za bahari, Bi. Oliva
Mkumbo akichangia hoja wakati wa kikao cha kamati tendaji cha mradi wa
ushirikiano wa SWIOFIC Nairobi Convention
kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha VETA Mkoani Tanga, Oktoba
04,2023.
Mkurugenzi Msaidizi wa
Uendelezaji wa Rasilimali za uvuvi, Idara ya Uvuvi Bi. Merisia Mparazo
akiwasilisha mada kwa wadau wa uvuvi (hawapo pichani) wakati wa kikao cha
kamati tendaji cha mradi wa ushirikiano wa SWIOFIC Nairobi Convention kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha VETA
Mkoani Tanga, Oktoba 04,2023.
Meneja wa Hifadhi za Bahari
na Maeneo Tengefu nchini Dkt. Immaculate Sware Semesi akichangia hoja wakati wa
kikao cha kamati tendaji cha mradi wa ushirikiano wa SWIOFIC Nairobi Convention
kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha VETA Mkoani Tanga, Oktoba 04,2023.
Afisa Uvuvi Mkuu kutoka
Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Tumaini Chambua
akiwasilisha mada wakati wa kikao cha kamati tendaji cha mradi wa
ushirikiano wa SWIOFIC Nairobi Convention
kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha VETA Mkoani Tanga, Oktoba
04,2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi
ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) Dkt. Ismael Kimirei (katikati) akiwa
kwenye picha ya pamoja na wawakilishi kutoka Shirika la Chakula na Kilimo
Duniani (FAO) , wawakilishi kutoka Nairobi Convention Secretariate na watendaji
kutoka Wizara ya mifugo na Uvuvi mara baada ya kikao cha kamati tendaji cha
mradi wa ushirikiano wa SWIOFIC Nairobi Convention kilichofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha VETA
Mkoani Tanga, Oktoba 04,2023.
Mratibu wa Mradi Kikanda
Bi. Ulrika Gunnartz akiwasilisha mada wakati wa kikao cha kamati tendaji cha
mradi wa ushirikiano wa SWIOFIC Nairobi Convention kilichofanyika kwenye ukumbi
wa chuo cha VETA Mkoani Tanga, Oktoba 04,2023.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni