◾ Wanawake watolewa na Mahakama
Timu ya kamba ya wanaume ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya SHIMIWI inayoendelea mkoani Iringa mara baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa mivuto yote miwili kwenye mchezo wao dhidi ya Wizara ya Afya uliochezwa leo Oktoba 06, 2023 kwenye uwanja wa Mkwawa.
Dalili ya ushindi katika mchezo huo ilianza kuonekana mapema ambapo Wizara ya Mifugo na Uvuvi iliuanza kwa kasi na kuthibitisha namna ilivyojipanga kubeba pointi kwenye mivuto yote.
Wakati huo huo timu ya kamba ya wanawake kutoka Wizarani hapo leo imeaga rasmi mashindano hayo baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya timu ngumu ya Mahakama kwenye mivuto yote miwili.
Wawakilishi wengine wa Wizara hiyo timu ya Mpira wa Miguu wanatarajia kutupa karata yao dhidi ya timu ya Wizara ya Mambo ya Ndani leo Oktoba 06, 2023 mchana kwenye uwanja wa Samora mkoani Iringa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni