Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2023

MIFUGO NA UVUVI YAIBAMIZA TUME YA UTUMISHI MPIRA WA PETE.

Picha
◾ Yatoa suluhu na Ofisi ya waziri Mkuu (Sera) upande wa mpira wa miguu.  Timu ya mpira wa pete kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza vema mbio za kutwaa taji la mchezo huo kwenye michuano ya SHIMIWI inayoendelea mkoani Iringa mara baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Tume ya Utumishi kwa magoli 11-6 kwenye mchezo uliochezwa chuo kikuu cha Ruaha leo Septemba 29, 2023. Timu hiyo ilianza kwa kasi ya chini kipindi cha kwanza ambapo hadi timu zinaenda mapumziko ilikuwa imeshakubali kichapo cha magoli 4-3 hali iliyomlazimu kocha wa timu hiyo Bi. Masele Shabani kufanya mabadiliko na kuiongezea kasi  timu hiyo hali iliyowafanya waibuke na ushindi huo mpaka mwisho wa mchezo. Kwa upande mwingine katika mchezo uliochezwa mapema kabisa leo asubuhi, timu ya Wizara hiyo kwa upande wa mpira wa miguu imetoka suluhu na timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera) mara baada ya kuhitimishwa kwa mchezo uliokuwa na upinzani mkali kutoka pande zote mbili. Timu hiyo inatarajia kutupa karata yake ya pili ...

WAZALISHAJI WA VYAKULA VYA MIFUGO WATAKIWA KUHAKIKI UBORA WA SAMPULI ZAO

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega ametoa rai na kuwasisitiza wazalishaji wa vyakula vya mifugo wote nchini kuhakikisha wanapeleka sampuli za vyakula wanavyozalisha kwenye maabara ya Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) ili kuhakiki ubora na viwango kwa kuzingatia matakwa ya sheria hiyo kabla ya kuanza kuwauzia wafugaji ndani ya nchi au kuvisafirisha nje ya nchi.  Waziri Ulega alitoa rai hiyo wakati akifungua warsha kuhusu uzalishaji wa protini kwa ajili ya vyakula vya Mifugo na kupunguza ushindani iliyofanyika jijini Dar es Salaam Septemba 29, 2023. Alisema kuwa tasnia hiyo imepewa kipaumbele na umuhimu wa pekee kwa kuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetunga sheria mahususi inayojulikana kwa jina la Sheria ya Maeneo ya Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Wanyama (Sura Na.180) pamoja na Kanuni na Miongozo mbalimbali. Lengo la sheria hiyo ni kuhakikisha vyakula vinavyozalishwa vinakidhi ubora na viwango stahiki ili kuwezesha uzalishaji bora wa mifugo, samaki na ...

MIFUGO NA UVUVI YAIBUKA KIDEDEA KAMBA WANAUME

Picha
Timu ya Wanaume kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza vema mbio zake za kutwaa ubingwa wa kuvuta kamba mara baada ya kuibuka na ushindi wa mivuto yote miwili dhidi ya timu ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwenye  mchezo uliochezwa leo Septemba 29, 2023 kwenye viwanja vya Chuo kikuu cha Mkwawa mkoani Iringa. Muda mfupi ujao Wizara itatupa karata yake kwa upande wa mpira wa miguu ambapo itamenyana na timu ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera) kwenye uwanja wa chuo kikuu cha Mkwawa. Timu ya mchezo wa kamba upande wa wanaume kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi ikimenyana na timu ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Lindi leo Septemba 29, 2023 ambapo iliibuka na ushindi wa mivuto yote miwili, Kulia ni mhamasishaji wa timu hiyo Bi. Mary Kamtole akitekeleza wajibu wake. Hiki ndio Kikosi cha mchezo wa Kamba kwa upande wa wanaume kilichoibuka na ushindi dhidi ya timu ya Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Lindi mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Chuo kikuu cha Mkwawa mkoani Iringa leo Septemba 29,2023 ikiwa ni sehem...

ULEGA AKIWAHUTUBIA WANAJUMUIYA YA WAISLAMU WA SUNNI KATIKA TUKIO LA KUADHIMISHA SIKUKUU YA KUZALIWA BWANA MTUME MUHAMMAD (S.A.W)

Picha
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akiwahutubia Wanajumuiya ya Waislamu wa Sunni katika tukio la kuadhimisha Sikukuu ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) liliyofanyika katika Msikiti wa Sunni jijini Dar es Salaam usiku wa Septemba 28, 2023. Katika tukio hilo, Waziri Ulega ndiye alikuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akiwa  na aliyewahi kuwa Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) wakishuhudia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika sherehe ya maadhimisho ya Sikukuu ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) iliyofanyika katika Msikiti wa Sunni jijini Dar es Salaam usiku wa Septemba 28, 2023. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (kushoto) akifurahia jambo na Mbunge wa Jimbo la Mpendae, Zanzibar, Mhe. Taufiq Turki walipokutana katika tukio la kuadhimisha Sikukuu ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) l...

MAADHIMISHO YA SIKU YA KICHAA CHA MBWA DUNIANI KITAIFA YAFANYIKA WILAYANI MPWAPWA

Picha
  Mkurugenzi msaidizi Idara ya Huduma za Afya ya Mifugo Dkt.Stanford Ndibalema Mwakilishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika Madhimisho ya ya siku ya Kichaa cha Mbwa Duniani  kitaifa Wilayani Mpwapwa akitoa Salamu za Wizara ambapo ameseama maadhimisho ya udhibiti wa Kichaa cha Mbwa nchini hufanyika kila mwaka kwa kushiikiana na Wizara ya Afya na wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kutoa elimu kwa jamii na wadau wa Mbwa na paka umuhimu wa kuchanja Mbwa ,(28.09.2023). Wadau wa Mbwa na paka walioleta mbwa wao kwa ajili ya kuchanjwa wakimsikiliza mgeni rasmi  hayupo pichani akisoma hatuba ya maadhimisho ya siku ya  kichaa cha Mbwa duniani Wilayani Mpwapwa .(28.09.2023) Mkurugenzi toka Wizara ya Afya Dkt.Rogati Kishimba akitoa salam za Wizara ya Afya kuhusu siku ya kichaa cha Mbwa duniani katika Madhimisho ya siku hiyo yaliyofanyika Wilayani Mpwapwa  leo ambapo amesema gharama za kutibu kichaa cha mbwa ni kubwa kuliko udhibi wa Ugonjwa huo hivyo jamii ihamasishwe kudhibit...

WAZIRI ULEGA AFANYA MAZUNGUMZO NA WATAALAM KUTOKA BENKI YA MAENDELEO YA AFRICA (AfDB)

Picha
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katika) akiongea na timu ya Wataalam kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) (hawapo pichani) alipokutana nao mapema leo Septemba 27, 2023 jijini Dodoma kwa lengo la kufanya tathmini ya awali ya mradi wa Jenga Kesho Iliyobora (BBT) ambao Benki hiyo wanataka kuunga mkono. Kulia ni Katibu Mkuu, Prof. Riziki Shemdoe na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Daniel Mushi. Mradi unatarajiwa kuanza Utekelezaji mapema mwezi Februari, 2024. Kiongozi wa Mradi kutoka Taasisi ya Mabadiliko ya Kilimo Afrika (AATI), Bw. Marin VanDamme (kulia) akimuonesha jambo Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega wakati wa kikao kilichofanyika ofisini kwa Waziri huyo jijini Dodoma mapema leo Septemba 27, 2023.  Lengo la kufika ofisini kwa Mhe. Waziri lilikuwa ni kuwasilisha hatua ya awali ya maandalizi ya Mpango Mkuu wa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kupata maoni ya Mhe. Waziri kwa hatua iliyofikiwa kabla ya kuendelea hatua inayofuata. Sehemu...

PROF. SHEMDOE AWAAGA WAWAKILISHI MICHUANO YA SHIMIWI

Picha
◾Waahidi Makubwa, Kuelekea Iringa kesho  Katibu Mkuu Wizara ya Mfugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe amewaaga wawakilishi wa wizara hiyo kwenye  michuano ya SHIMIWI ambapo amewataka wawakilishi hao kurejea na ushindi wa nafasi ya kwanza kwenye kila mchezo watakaoshiriki. Katika tukio hilo lililofanyika Septemba 27, 2023 kwenye Ofisi ndogo za Wizara hiyo zilizopo jengo la NBC jijini Dodoma, Prof. Shemdoe amewataka wachezaji wote waliochaguliwa kushiriki kwenye michuano hiyo kujituma na kucheza kwa ushindani wakati wote wa michuano hiyo. “Mimi mara zote nipo kwenye timu ya ushindi kwa hiyo hata huku naamini nimekuja kwenye timu ya ushindi na nina Imani sana na nyinyi kwa sababu ninafahamu kuwa kwenye mashindano ya mwaka huu tutakuwa na vikombe vingi zaidi ya vile tulivyoshinda mwaka jana” Ameongeza Prof. Shemdoe. Akisisitiza suala la kudumisha  nidhamu , Prof Shemdoe amewataka wachezaji hao kutambua kuwa wao ni watumishi wa umma hivyo wanapaswa kufuata taratibu zote zinazowao...

KONGAMANO LA WADAU WA MAZIWA LAFANYIKA MKOANI MWANZA

Picha
  Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania Dkt. George Msalya akitoa neno la utangulizi kwenye Kongamano la Wadau wa Maziwa mkoa wa Mwanza lilifanyika Septemba 26, 2023 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ambapo ameelezea ukuaji wa Sekta ya Maziwa kwa ujumla hivyo amewataka wananchi wa Mwanza kuchangamkia fursa zilizopo kwenye Ufugaji hasa wa Ng'ombe wa Maziwa. Mwakilishi wa Shirika la Heifer International Bw. Ndisha Joseph akijibu moja ya hoja iliyoibuka kwenye Kongamano la Wadau wa Maziwa lililofanyika Septemba 26, 2023 jijini Mwanza ambapo mmoja wa wajumbe alitaka kujua namna shirika hilo linavyoweza kuwasaidia wafugaji wadogo wadogo wa ng'ombe wa maziwa kupata elimu ili kufahamu faida ya kuwa katika vikundi vya Ushirika Sehemu ya Washiriki wa Kongamano la Wadau wa Maziwa lililofanyika Septemba 26, 2023 Mkoani Mwanza wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye Kongamano hilo ambapo sehemu kubwa ya walioalikwa ni Wakuu wa Shule na Walimu Wa...

KIKAO KAZI

Picha
  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega(kulia) akiongea na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti katika kikao kazi kilichofanyika ofisini kwake jijini Dodoma mapema leo Septemba 26, 2023. Katika kikao hicho, pamoja na mambo mengine walijadiliana kuhusu dira na muelekeo wa utekelezaji wa majukumu na shughuli mbalimbali za kila siku za Wizara katika kuwahudumia wananchi na kutimiza maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) akimueleza jambo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Alexander Mnyeti katika kikao kazi kilichofanyika ofisini kwake jijini Dodoma mapema leo Septemba 26, 2023. Katika kikao hicho pamoja na mambo mengine walijadiliana kuhusu dira na muelekeo wa utekelezaji wa majukumu na shughuli mbalimbali za kila siku za Wizara katika kuwahudumia wananchi na kutimiza maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Wengine ka...

BI. MEENA AFUNGUA KIKAO KILICHOJADILI MRADI WA TASFAM

Picha
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Kisaka Meena, akifungua kikao cha Menejimenti cha kupitia nyaraka muhimu za Mradi wa TASFAM ulioudhuriwa na wakuu wa Idara, Vitengo na wajumbe wengine muda mfupi baada ya kufika kwenye ukumbi wa wizara Septemba 25, 2023. Sehemu ya washiriki wa kikao cha Menejimenti cha kupitia nyaraka muhimu za Mradi wa TASFAM wakimsikiliza kwa makini Naibu Katibu Mkuu Sekta ya Uvuvi Bi. Agness Meena (hayupo pichani) wakati akifungua kikao hicho kwenye ukumbi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi mtumba jijini Dodoma  Septemba 25,2023. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Kisaka Meena (wa sita kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Sekta ya Uvuvi iliyokutana kujadili nyaraka muhimu za Mradi wa TASFAM ulioudhuriwa na wakuu wa Idara, vitengo na wajumbe wengine katika ukumbi wa Wizara Septemba 25, 2023.

BOTI 4 ZENYE THAMANI YA 200M ZAKABIDHIWA KWA BMU's NKASI

Picha
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe leo tarehe 25 Sept 2023 amezindua na kukabidhi boti nne za doria zenye thamani ya 200M zilizotolewa msaada na taasisi ya The Nature Conservancy (TNC) kwa BMU's tisa zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa. Akikabidhi boti hizo Prof.Shemdoe amesema kuwa boti hizo zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa, boti hizo ni kwaajili ya matumizi ya doria tu zisionekane tena  zinafanya kazi kinyume na malengo yaliyokusudiwa. "Boti hizi nazizindua leo na kuwakabidhi, naomba sana zikatumike kwa ajili ya doria,zisionekane tena zinavua samaki huko ziwani, BMU's mnatakiwa kuwa waaminifu,mzitumie hizi boti kwa maslahi ya Jamii nzima inayowazunguka hapa". Alisema Prof.Shemdoe. Aidha, Vijiji nufaika na Boti hizo ni pamoja na Kalungu, Mkinga, Kilando na Itete. Pia, Katibu Mkuu amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali wa Wavuvi kote nchini, kwani katika ...

ELIMU YA KUENDESHA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA YATOLEWA

Picha
  Bw. Imani Mwakalile kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), akitoa elimu ya namna ya kuendesha kituo cha huduma kwa wateja ambacho kinatarajia kuanzishwa kwa lengo la kuwahudumia wadau wa sekta ya Mifugo na Uvuvi, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa NBC, Dodoma, 21.09.2023. Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani Dkt. Angelo Mwilawa(aliyesimama) akifungua kikao cha kujadili namna ya kuendesha kituo cha huduma kwa wateja(Call Centre Service), ambacho kinatarajiwa kuanzishwa Wizarani, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa NBC, Dodoma, 21.09.2023. Wajumbe wa kikao cha kujadili namna ya kuendesha kituo cha huduma kwa wateja kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi,  wakimsikiliza mwezeshaji Bw.Imani Mwakalile, kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL- aliyesimama) katika ukumbi wa NBC, Dodoma 21.09.2023. Mwakilishi kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) (katikati) Bw. Imani Mwakalile akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya Mifugo n...

​RAIS, DKT. SAMIA AANDIKA HISTORIA MPYA SEKTA YA UVUVI

Picha
Leo Septemba 19, 2023, ni siku ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameandika historia mpya katika sekta ya uvuvi baada ya kuweka jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Bandari ya Uvuvi ya Kilwa Masoko ambayo haijawahi kuwepo tangu nchi ya Tanzania ipate uhuru. Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka  jiwe hilo la msingi la ujenzi wa bandari ya uvuvi ya Kilwa katika tukio lililofanyika Wilayani Kilwa, Mkoani Lindi ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika Mikoa ya Mtwara na Lindi. Kukamilika kwa bandari hiyo kutawezesha meli za uvuvi zinazovua katika Ukanda wa Uchumi wa Bahari ya Tanzania na Bahari Kuu kutia nanga na kushusha samaki wanaolengwa na wale wasiolengwa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.  Pia, uwepo wa bandari ya uvuvi utachochea uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vya kuchakata samaki na miundombinu ya uhifadhi wa mazao ya uvuvi. Hivyo, uwekezaji huu, unaenda kuimarisha biashara ya mazao ya uvuvi kwenda nje ya...

HAFLA YA UWEKEAJI WA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BANDARI YA UVUVI NA UGAWAJI WA BOTI ZA UVUVI

Picha
 

BBT KUTATUA CHANGAMOTO YA BEI YA NYAMA MTWARA

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema kuwa wizara yake imejipanga kutumia Shamba la Mifugo la Nangaramo lililopo Mkoani Mtwara kuanzisha programu ya BBT ili kuwapa fursa vijana wa Mikoa ya Kusini kunenepesha mifugo na kuuza nyama kwa bei nafuu tofauti na ilivyo sasa mkoani Mtwara bei ya kilo moja ya nyama inafika mpaka Shilingi Elfu Kumi (10000). Waziri Ulega aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Wananchi wa Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara leo Septemba 17, 2023. Alisema pamoja na uwepo wa mifugo mingi katika Mkoa huo na Mikoa mingine ya jirani lakini bado upatikanaji wa nyama kwa bei nafuu umekuwa changamoto na ndio maana wamejipanga kuanzisha programu ya BBT itakayowawezesha vijana kunenepesha mifugo na kuuza nyama kwa bei ambayo wananchi walio wengi wataimudu. Aliongeza kwa kusema kuwa kupitia programu hiyo vijana pia wataweza kunufaika na kuuza mifugo na nyama kwa nchi ya Comoro ambayo k...