WATAALAMU WATAKIWA KUKUSANYA TAKWIMU SAHIHI ZA KITAFITI
Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Saame amewataka wataalamwa Sekta ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha wanachukua takwimu sahihi wakati wa kukusanyataarifa za kitafiti ili ziweze kuisaidia Serikali katika kupanga mipango yake. Waziri Shaame ameyasema hayo wakati akifunga Kongamano la 46 la Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Mkutano Mkuu wa 47 wa Mwaka wa Chama cha Wataalamu wa Uzalishaji na Uendelezaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) lililofanyika kwenye Ukumbi wa Olasit Garden, Arusha Oktoba 27, 2023. "Takwimu sahihi kuhusu taarifa za mifugo na uvuvi zitasaidia kutunga sera, kunyoosha maono, fikra na miongozo ya ilani ya chama cha mapinduzi kuweza kufikia malengo ya kuwainua wananchi kupata mafanikio kwa haraka," alisema Aliongeza kwa kusema kuwa Serikali inawategemea sana wataam na hivyo watumie vizuri teknolojia walizonazo ili zikaboreshe tasnia nzima ya ufugaji ili kupata maendeleo. “Wizara ...
.jpeg)
Maoni
Chapisha Maoni