Bw. Imani Mwakalile kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), akitoa elimu ya namna ya kuendesha kituo cha huduma kwa wateja ambacho kinatarajia kuanzishwa kwa lengo la kuwahudumia wadau wa sekta ya Mifugo na Uvuvi, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa NBC, Dodoma, 21.09.2023.
Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani Dkt. Angelo Mwilawa(aliyesimama) akifungua kikao cha kujadili namna ya kuendesha kituo cha huduma kwa wateja(Call Centre Service), ambacho kinatarajiwa kuanzishwa Wizarani, kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa NBC, Dodoma, 21.09.2023.
Wajumbe wa kikao cha kujadili namna ya kuendesha kituo cha huduma kwa wateja kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, wakimsikiliza mwezeshaji Bw.Imani Mwakalile, kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL- aliyesimama) katika ukumbi wa NBC, Dodoma 21.09.2023.
Mwakilishi kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) (katikati) Bw. Imani Mwakalile akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi kutoka wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambao wameshiriki kwenye kikao cha kujadili namna ya kuendesha kituo cha huduma kwa wateja (Call Centre Service) ambacho kinatarajia kuanzishwa kwa lengo la kuwahudumia wadau wa sekta ya uvuvi na Mifugo, katika ukumbi wa NBC, Dodoma, 21.09.2023.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni