Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amesema kuwa wizara yake imejipanga kutumia Shamba la Mifugo la Nangaramo lililopo Mkoani Mtwara kuanzisha programu ya BBT ili kuwapa fursa vijana wa Mikoa ya Kusini kunenepesha mifugo na kuuza nyama kwa bei nafuu tofauti na ilivyo sasa mkoani Mtwara bei ya kilo moja ya nyama inafika mpaka Shilingi Elfu Kumi (10000).
Waziri Ulega aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Wananchi wa Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara leo Septemba 17, 2023.
Alisema pamoja na uwepo wa mifugo mingi katika Mkoa huo na Mikoa mingine ya jirani lakini bado upatikanaji wa nyama kwa bei nafuu umekuwa changamoto na ndio maana wamejipanga kuanzisha programu ya BBT itakayowawezesha vijana kunenepesha mifugo na kuuza nyama kwa bei ambayo wananchi walio wengi wataimudu.
Aliongeza kwa kusema kuwa kupitia programu hiyo vijana pia wataweza kunufaika na kuuza mifugo na nyama kwa nchi ya Comoro ambayo kwa kiasi kikubwa wanategemea biashara Mifugo na nyama kutoka nchini Tanzania.
Halikadhalika alisema kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi imejipanga pia kutumia maeneo yote yaliyopo katika mpango wa matumizi bora ya ardhi kuweka miundombinu ya kisasa ya mifugo ili kuwawezesha wafugaji kuzalisha kwa tija.
Aidha, Waziri Ulega alimshukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo yake juu ya migogoro ya wakulima na wafugaji iliyopo katika Mikoa ya Kusini na kumuahidi kwamba watasimamia vyema maelekezo yake huku akiongeza kwa kuwataka wafugaji kuhakikisha wanafanya ufugaji wao kwa kuzingatia Sheria za nchi na atakayeendelea kukiuka hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (kulia) akifurahia jambo na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Jerry Silaa alipokutana nae katika tukio la uzinduzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Septemba 15, 2023.
Sehemu ya Wananchi mkoani Mtwara wakiwa wamejitokeza kumlaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa tukio la uzinduzi wa Barabara ya Mtwara – Mnivata (Kilometa 50) leo Septemba 15, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali muda mfupi baada ya kuwasili kwa ajili ya tukio la kukagua na kuona shughuli za uboreshaji wa Bandari ya Mtwara leo Septemba 15, 2023. Wa tatu kutoka kulia anayesalimiana nae ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Viongozi wengine wakati wa tukio la kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Septemba 15, 2023. Wa tatu kutoka kulia ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (kushoto) akijadiliana jambo na Mbunge wa Mtwara Mjini, Mhe. Hassan Mtenga alipokutana nae katika Mkutano wa hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mkoani Mtwara Septemba 15, 2023.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (kushoto) akiongea na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Cde. Mohamed Kawaida alipokutana nae katika Mkutano wa hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan uliofanyika kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mkoani Mtwara Septemba 15, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongea na Wananchi wa Mkoa wa Mtwara katika Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mkoani Mtwara Septemba 15, 2023. Wa kwanza kulia waliokaa ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni