SERIKALI KUKOPESHA WANAWAKE SEKTA YA MIFUGO NA UVUVI
Serikali kupitia Benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya (EIB) inatarajia kutoa mkopo wa Sh1.3 trilioni kusaidia wanawake kuboresha biashara na uwekezaji kwenye mnyororo wa thamani katika sekta za mifugo na uvuvi. Akizungumza kuhusu fursa hiyo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya mifugo na uvuvi Dkt. Daniel Mushi alisema dhumuni la fedha hiyo ni kuwezesha sekta binafsi kuwa kichocheo cha maendeleo, Machi 21, 2023 “Kwa kuanzia walengwa mahsusi ni sekta binafsi hususan kwa biashara zinazoongozwa na wanawake au shughuli zinazoambatana na uchumi wa buluu ikiwemo kilimo cha mwani”alisema Dkt. Mushi. Aidha Dkt. Mushi alisema sio tu kuwainua wanawake katika uwekezaji bali hata kuzalisha fursa za ajira kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya bahari na mifugo kwa ujumla na kupunguza suala la ukosefu wa ajira nchini. “Wajasiriamali watumie fursa hii vizuri ili iwe kioo na baadae tuaminike ili fedha zijazo zipitie moja kwa moja kwenye sekta binafsi na fursa hii itakuja tena ikiwa tutakuwa waaminifu kw...