NZUNDA ATOA MAELEKEZO KWA WATAFITI WA MIFUGO
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Tixon Nzunda amewataka watafiti wa mifugo kufanya tafiti zinazozingatia maslai ya nchi. Nzunda ameyasema hayo (20.02.2023) wakati akifungua Warsha ya Uzinduzi wa Mradi wa Utafiti wa Mifugo na Mazingira kwa lengo la kuchunguza utoaji wa jopo gesi (GHC) na kupunguza gharama za chakula katika mifumo ya wafugaji wadogo wa ng’ombe wa maziwa iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Panama mkoani Kilimanjaro. Watafiti wametakiwa kuzingatia malengo ya nchi katika kuleta mabadiliko kwenye sekta ya mifugo katika tafiti wanazozifanya ili kuongeza tija katika uzalishaji na sio kutumia tafiti hizo kwa matakwa ya wafadhili au maslai yao binafsi. Pia watafiti wametakiwa kuzingatia utaalam, misingi ya maadili, uwajibikaji unaotokana na matendo na matokeo ya tafiti wanazozifanya ukiwemo utafiti wa Mifugo na Mazingira kwa lengo la kuchunguza utoaji wa jopo gesi (GHC) na kupunguza gharama za chakula katika mifumo ya wafuga...