Wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi wakishirikiana na mmoja wa wafugaji (katikati) kupima katika mzani kiasi cha mbegu kwa ajili ya kuziandaa ili zipandwe katika shamba la mfugaji lililopo katika Kata ya Itiso, Wilayani Chamwino, Mkoani Dodoma Februari 14, 2023.
Sehemu ya Wafugaji na Viongozi wa Kata ya Itiso, Wilayani Chamwino, Mkoani Dodoma wakishiriki katika zoezi la upandaji wa malisho ya mifugo baada ya kupatiwa mafunzo na wataalam kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhusu umuhimu wa kupanda malisho kwa ajili ya mifugo yao. Elimu hiyo ilitolewa Februari 14, 2023.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho na Rasilimali ya Vyakula vya Wanyama, Dkt. Asimwe Rwiguza (kushoto) akiongea na wafugaji wa Kata ya Itiso, Wilayani Chamwino, Mkoani Dodoma Februari 14, 2023 alipowatembelea kwa lengo la kuwahamasisha kuhusu ulimaji wa malisho ili waondokane na utegemezi wa malisho ya asili jambo ambalo limekuwa likipelekea migogoro kati yao na watumiaji wengine wa Ardhi.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho na Rasilimali ya Vyakula vya Wanyama, Dkt. Asimwe Rwiguza akishirikiana na wafugaji wa Kata ya Itiso, Wilayani Chamwino, Mkoani Dodoma kupanda malisho ya mifugo katika shamba la mmoja wa wafugaji wa Kata hiyo alipowatembelea Februari 14, 2023 kwa lengo la kuwahamasisha kuhusu ulimaji wa malisho ili waondokane na utegemezi wa malisho ya asili jambo ambalo limekuwa likipelekea migogoro kati yao na watumiaji wengine wa Ardhi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni