Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Tixon Nzunda amewataka watafiti wa mifugo kufanya tafiti zinazozingatia maslai ya nchi.
Nzunda ameyasema hayo
(20.02.2023) wakati akifungua Warsha ya Uzinduzi wa Mradi wa Utafiti wa Mifugo
na Mazingira kwa lengo la kuchunguza utoaji wa jopo gesi (GHC) na kupunguza
gharama za chakula katika mifumo ya wafugaji wadogo wa ng’ombe wa maziwa
iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Panama mkoani Kilimanjaro.
Watafiti wametakiwa
kuzingatia malengo ya nchi katika kuleta mabadiliko kwenye sekta ya mifugo
katika tafiti wanazozifanya ili kuongeza tija katika uzalishaji na sio kutumia
tafiti hizo kwa matakwa ya wafadhili au maslai yao binafsi.
Pia watafiti
wametakiwa kuzingatia utaalam, misingi ya maadili, uwajibikaji unaotokana na matendo
na matokeo ya tafiti wanazozifanya ukiwemo utafiti wa Mifugo na Mazingira kwa
lengo la kuchunguza utoaji wa jopo gesi (GHC) na kupunguza gharama za chakula
katika mifumo ya wafugaji wadogo wa ng’ombe wa maziwa.
Vilevile amewasihi
watanzania kuziunga mkono taasisi za utafiti kwa kuwa sayansi huwa haisemi
uongo, hivyo kupitia tafiti hizo mabadiliko kwenye sekta ya mifugo.
Nzunda amewataka
maafisa ugani kuhakikisha wanayafikisha matokeo ya tafiti kwa wafugaji na
kuhakikisha yanatumika. Aidha, maafisa ugani wametakiwa kuhakikisha
wanawatembelea wafugaji na kutoa ushauri wao pale unapohitajika. Vilevile
ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa kuweka utaratibu wa kuwapima maafisa
hao ili kuhakikisha wafugaji wanatembelewa.
Akiuzungumzia mradi
huo, Mratibu wa mradi wa ADGG na
Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Duniani (ILRI), Dkt. Eliamoni Lyatuu
amesema kuwa taasisi hiyo ya utafiti imekuwa ikifanya tafiti mbalimbali hapa
duniani kwa kushirikiana na taasisi za utafiti za nchi husika.
Katika mradi huo,
wamelenga kufanya utafiti utakaosaidia kuangalia athari za mazingira
zinazosababishwa na mifugo, lengo likiwa ni kuhakikisha kuna kuwa na ufugaji wa
ng’ombe kwa gharama nafuu na usioathiri mazingira.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Tixon Nzunda akifungua Warsha ya Uzinduzi wa Mradi wa Utafiti wa Mifugo na Mazingira kwa lengo la kuchunguza utoaji wa gesi joto (GHC) na kupunguza gharama za chakula katika mifumo ya wafugaji wadogo wa ng’ombe wa maziwa iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Panama mkoani Kilimanjaro ambapo amewasihi watafiti hao kuzingatia malengo ya nchi katika kuleta mabadiliko kwenye sekta ya mifugo katika tafiti wanazozifanya ili kuongeza tija katika uzalishaji. (20.02.2023)
Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Huduma za Ugani, Dkt. Dkt. Angello Mwilawa akizungumza wakati wa Warsha ya Uzinduzi wa Mradi wa Utafiti wa Mifugo na Mazingira kwa lengo la kuchunguza utoaji wa gesi joto (GHC) na kupunguza gharama za chakula katika mifumo ya wafugaji wadogo wa ng’ombe wa maziwa iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Panama mkoani Kilimanjaro ambapo alielezea namna wizara inavyoshirikiana na taasisi za utafiti wa mifugo. (20.02.2023)
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti Tanzania, Prof. Erick Komba akieleza malengo ya taasisi hiyo katika kuhakikisha wafugaji wananufaika na tafiti mbalimbali zinazofanyika ili waweze kufuga kwa tija wakati wa Warsha ya Uzinduzi wa Mradi wa Utafiti wa Mifugo na Mazingira kwa lengo la kuchunguza utoaji wa gesi joto (GHC) na kupunguza gharama za chakula katika mifumo ya wafugaji wadogo wa ng’ombe wa maziwa iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Panama mkoani Kilimanjaro. (20.02.2023)
Mratibu wa mradi wa ADGG na Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Duniani, Dkt. Eliamoni Lyatuu akitoa maelezo kwa washiriki kabla ya kufanyika kwa kazi za makundi wakati wa Warsha ya Uzinduzi wa Mradi wa Utafiti wa Mifugo na Mazingira kwa lengo la kuchunguza utoaji wa gesi joto (GHC) na kupunguza gharama za chakula katika mifumo ya wafugaji wadogo wa ng’ombe wa maziwa iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Panama mkoani Kilimanjaro. (20.02.2023)
Mratibu wa mradi wa ADGG na Mtafiti wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Duniani, Dkt. Eliamoni Lyatuu akitoa maelezo kwa washiriki kabla ya kufanyika kwa kazi za makundi wakati wa Warsha ya Uzinduzi wa Mradi wa Utafiti wa Mifugo na Mazingira kwa lengo la kuchunguza utoaji wa gesi joto (GHC) na kupunguza gharama za chakula katika mifumo ya wafugaji wadogo wa ng’ombe wa maziwa iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Panama mkoani Kilimanjaro. (20.02.2023)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni