Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2022

UGAWAJI WA MADUME BORA YA NG’OMBE NI UTEKELEZAJI WA MPANGO WA MABADILIKO WA SEKTA YA MIFUGO - NDAKI

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amesema ugawaji wa madume ya bora ya ng’ombe ni utekelezaji wa mpango wa mabadiliko wa Sekta ya Mifugo.   Waziri Ndaki ameyasema hayo leo (24.11.2022) wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wakati alipokuwa anagawa madume bora 50 ya ng’ombe aina ya boran ambapo kila mmoja ana uwezo wa kupanda majike 25 kwa mwaka, kwa vikundi vya wafugaji kwa lengo la kwenda kuboresha mifugo yao ambayo mingi ni ya asili.   “Mifugo mingi iliyopo hapa nchini ni ya asili na uzalishaji wake wa nyama na maziwa kwa mfugo ni ndogo, hivyo kwa kuanza kuboresha mifugo kwa kutumia madume haya pamoja na njia ya uhimilishaji kutasaidia wafugaji kuwa na mifugo michache ambayo itakuwa na uzalishaji mkubwa wa nyama na maziwa,” Alisema   Ng’ombe wa asili huzalisha nyama kilo 80 -120 kwa ng’ombe wakati baada ya kuboreshwa kwa kosaafu mfugaji anaweza kupata kilo 150 – 200 kwa ng’ombe. Lakini pia kwenye upande wa maziwa ng’ombe hawa walioboreshwa kosaafu huwa na uwezo w...
Picha
  Mtaalam Mwandamizi wa Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji kutoka Mfuko wa kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Bw. Richard Abila (kulia) akimpa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki (katikati) tathmini fupi ya yale waliyoyaona kwenye utekelezaji wa awali wa Mradi wa Maendeleo ya Kilimo na Uvuvi (AFDP) hapa nchini tukio lililofanyika mapema leo (24.11.2022) kwenye Ofisi za Wizara hiyo zilizopo eneo la Mtumba jijini Dodoma. Kushoto ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi Bw.Stephen Lukanga.

TVLA YATOA CHANJO KWA BAADHI YA WAFUGAJI WA KUKU WILAYANI BAHI

Picha
  Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Kanda ya Kati Dkt. Japhet Nkagaga wa (kwanza kulia) mwenye boksi la plastiki la kuhifadhia chanjo  za mifugo, akitoa chanjo kwa ajili ya kuchanja Mifugo na pia ametoa elimu kwa moja ya Kikundi  cha wafugaji wa kuku katika Kijiji cha Ilindi Wilayani Bahia,ambapo amewataka wafugaji hao kuona   umuhimu wa kuchanja kuku kutumia chanjo ya I-2 dhidi ya ugonjwa Kideri ili kuwanusuru na vifo vya kuku wao  katika Kikundi chao,ambapo ugonjwa huo ukiingia katika kaya ya mmoja wenu unauawa kuku takriban wote katika kaya.Lengo la kutoa elimu hii ni utaratibu wa Wakala ya  Maabara ya veterinari kanda ya Kati waliojiwekea wa kutoa huduma ya afya ya Mifugo kwa wafugaji  kanda hiyo katika kuadhimisha Wiki ya Wakala ya Maabara ya Veterinari kanda ya Kati  Dodoma.(23.11.2022). Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Kanda ya Kati Dodoma Dkt.Japhet Nkagaga akichanja Ng'ombe katika Kijiji cha Ilindi Kata ya Ilindi Wil...

UZINDUZI WA MRADI WA "MAZIWA FAIDA TANZANIA"

Picha
 

MBEGU ZA MALISHO ZIPATIKANE KWENYE MADUKA YA PEMBEJEO-ULEGA.

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Mifugo nchini (TALIRI) kuhakikisha mbegu za malisho bora ya Mifugo zinapatikana kwenye maduka ya pembejeo za Kilimo na Mifugo ili kuwawezesha wafugaji kuzalisha malisho kwa urahisi zaidi. Mhe. Ulega ameyasema hayo kwenye hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Faida Maziwa Tanzania uliofanyika jana (22.11.2022) kwenye Viwanja vya Ofisi za Taasisi hiyo kanda ya Mashariki zilizopo jijini Tanga. "Moja ya jambo ambalo litatupa heshima kubwa sana ni kuhakikisha mbegu za malisho zinauzwa kama zilivyo mbegu za mazao mengine kama mahindi, mpunga na mengineyo kwa sababh tunatumia nguvu kubwa sana kuwahamisha wafugaji kuzalisha malisho bora kwa ajili ya Mifugo yao lakini mbegu za malisho hayo hazipatikani kwa urahisi hivyo ni muhimu sasa zikaanza kupatikana kwenye maduka yote ya pembejeo na hilo ninaagiza lifanyike haraka sana" Amesisitiza Mhe. Ulega. Mhe. Ulega amebainisha kuwa hatua hiyo ikifikiwa, Nchi itakuwa ...

MAADHIMISHO YA WIKI YA TVLA

Picha
 
Picha
  Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (wa pili kutoka kulia, mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Wizara mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwenye mkutano wa siku mbili wa Makatibu Wakuu (Committee of Senior Officials) wa Jumuiya ya IORA  unaofanyika Jijini Dhaka, Bangladesh kuanzia Novemba 22-23, 2022. Dkt. Tamatamah ameongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo ambao unatarajiwa  kuhitimishwa na kikao cha Baraza la Mawaziri kitakachofanyika Novemba 24, 2022. Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Baraza la Mawaziri utaongozwa na Mhe. Suleiman Masoud Makame, Waziri wa Uchumi wa Buluu na  Uvuvi wa SMZ. Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akitoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya hoja zilizojitokeza kuhusu Tanzania kwenye mkutano wa siku mbili wa Makatibu Wakuu (Committee of Senior Officials) w...

KONGAMANO LA PILI LA KITAIFA LA WADAU LA KUJADILI NAMNA YA PAMOJA YA KUZUIA USUGU WA VIMELEA VYA MAGONJWA DHIDI YA DAWA

Picha
  Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Prof. Hezron Nonga akitoa neno la utangulizi wakati wa Kongamano la pili la Kitaifa la wadau la  kujadili  namna ya pamoja ya kuzuia usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 22-23, 2022. Kongamano hilo ni miongoni mwa matukio ya Wiki ya kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu usugu wa vimelea dhidi ya dawa  iliyoanza Novemba 18-23, 2022. Kongamano hilo limeandaliwa na Wizara ya Afya, Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Vyuo Vikuu, Taasisi za Utafiti na Wadau wa Maendeleo. Sehemu ya Wadau wa  Kongamano la Kitaifa la  kujadili namna ya pamoja ya kuzuia usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa wakifuatilia matukio mbalimbali yanayoendelea  katika kongamano hilo linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 22-23, 2022. Pichani ni muonekano wa sehemu ya ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania ambapo Kongamano la pili la Ki...

SERIKALI YAPONGEZA SEKTA BINAFSI KWA KUKUZA SEKTA YA UVUVI

Picha
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imelipongeza Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF) kwa kuviwezesha vikundi saba vya ujasiriamali vya uvuvi kwa jumla ya Shilingi Milioni Thelathini na Tano, pikipiki nne, boti tatu na injini zake, pamoja na makoti 30 ya kujiokoa (life jackets) kwa halmashauri mbili za Wilaya za Kilwa Mkoani Lindi na Kibiti Mkoani Pwani. Shukrani hizo zimetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatamah katika hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji, Bw. Anthony Dadu wakati wa maadhimisho ya siku ya mvuvi duniani yanayokwenda sambamba na Mwaka wa Kimataifa wa Wavuvi Wadogo na Wakuzaji Viumbe Maji 2022 (International Year of Artisanal Fisheries and Aquaculture (IYAFA) yaliyofanyika katika kijiji cha Somanga Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi. Amesema hatua hiyo itaongeza chachu ya usimamizi bora wa rasilimali za uvuvi utakaopelekea upatikanaji...

SERIKALI YAFANYA MAGEUZI KWENYE SEKTA YA MIFUGO

Picha
Na. Martha Mbena. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki amesema Serikali kupitia Wizara ya Mifugo imekuja na mageuzi kwa kufuga mifugo bora yenye tija kupitia Ng'ombe aina ya Borani ili kupata kilo nyingi, nyama nyingi na kuzalisha maziwa mengi jambo ambalo litachangia pato la Taifa. Waziri Ndaki ameyasema hayo (21.11.2022) wakati akikabidhi madume 50 ya Ng'ombe aina ya Borani kwa makundi ya wafugaji wa Wilaya ya Maswa  kwenye hafla fupi iliyofanyika kwenye kata ya Buchambi Mkoani Simiyu. "Kiasi cha sh 915 milioni kilichotolewa na Serikali kimetumika kununua madume 336 ya Ng'ombe aina ya Borani  ambayo yatakabidhiwa kwenye Wilaya 10 nchi nzima, Kwa hapa Wilaya ya Maswa tumekabidhi haya madume 50, Ombi langu muwatunze kwa kuwaosha mara kwa mara ili wasipate kupe wakapata ugonjwa wa Ndigana," Alisema Waziri Mashimba. Mhe. Mashimba  aliongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa Ng'ombe hao bure kwa vikundi vyote vya wafugaji na kila kikundi kitapata dum...

TVLA KANDA YA KATI YATOA ELIMU YA KWA WAFUGAJI

Picha
  Meneja Wakala ya Maabara ya Mifugo Tanzania ( TVLA ) kanda ya kati Dodoma Dkt.Japhet Joas Nkangaga akiwa ofisini kwake Dodoma ameleza ratiba watakavyo tekeleza utoaji elimu kwa wafugaji katika maadhimisho ya wiki TVLA ni pamoja na kesho tarehe 22.11.2022 wataenda kutoa elimu  Halmashauri ya Dodoma vijijini,shule ya Amani,Mlezi na Kilimani.Tarehe 23.11.2022 timu ya wataalam itakuwa Hamashauri ya Bahi kuchanja Mifugo ya wafugaji na 24.11.2022 timu hiyo ya wataalam itakuwa Dodoma Jiji kuchukua sampuli ili kuchunguza magonjwa mbalimbali CBPP na kuchanja kuku dhidi ya ugonjwa wa Kideri. (21.11.2022) Baadhi ya Wataalam wa TVLA Kanda ya kati wakiongozwa na Dkt.Harrison Gabriel  kushoto wakiwa na mteja wao ambaye amekuja kupa huduma ya elimu ya uchanjaji kuku dhidi ya kideri cha kuku leo katika ofisi za TVLA Kanda ya kati.Kauli Mbiu ya Maadhimisho hayo ni,"Tambua,Tibu na Udhibiti wa magonjwa ya Mifugo".( 21.11.2022 ) Maadhimisho ya wiki ya TVLA Kanda ya kati yameanza leo.ambapo...

MAABARA ZA TVLA SASA ZAFANYA KAZI KIDIGITALI

Picha
Na Mbaraka Kambona, Wakala ya Maabara ya Mifugo Tanzania (TVLA) imewezeshwa vifaa vya kisasa katika maabara zake ambapo sasa wamekuwa na  uwezo wa kutambua kwa haraka vimelea vya magonjwa ya mifugo ndani ya dakika 15 tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa inawachukua kati ya masaa 24 hadi 36. Hayo yamefahamika  leo Novemba 21, 2022, jijini Dar es Salaam wakati  Mwakilishi kutoka Taasisi ya American Society for Microbiology, Dkt. Wes Kim akimkabidhi  Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo), Prof. Hezron Nonga nyaraka za vifaa vya maabara ambavyo vimegharimu zaidi ya Shilingi za Kitanzania Milioni 600. Akizungumza baada ya makabidhiano hayo, Prof. Nonga alisema kuwa lengo la kuboresha maabara hizo ni kuzijengea uwezo hasa kwenye kubaini uwepo wa vimelea ambavyo vimepelekea matumizi makubwa ya dawa za antibayotiki kwenye mifugo hasa kuku. “Kutokana na mazingira tuliyonayo Tanzania, uwepo wa vimelea haukwepeki kutokana na joto, mvua na hali ya unyevuny...

ULEGA: TUMIENI TEHAMA KUWAFIKIA WAFUGAJI

Picha
Na. Edward Kondela Wataalamu wa mifugo nchini wametakiwa kuhakikisha wanatumia vyema Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuwafikia wafugaji wengi na kutatua changamoto zao. Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amebainisha hayo (18.11.2022) katika Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza, wakati akifunga mafunzo rejea ya baadhi ya wataalamu wa mifugo kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoa kutoka Kanda ya Ziwa Magharibi inayohusisha mikoa ya Mwanza, Kagera na Geita yaliyoandaliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, akisema kuwa idadi ya wataalamu wa mifugo waliopo nchini kwa sasa haitoshelezi kila mfugaji kufikiwa na mtaalamu kwa wakati. Naibu Waziri Ulega ameongeza kuwa kutokana na ukuaji wa tekonolojia wafugaji wengi wanatumia simu za mkononi hivyo zikitumika vyema kwa kushirikiana na wataalamu wa mifugo kupitia mfumo wa M-Kilimo kwa ajili ya huduma za ugani itakuwa ni njia rahisi kwa wafugaji kutatuliwa changamoto zao kwa haraka zaidi na kupata ushauri wa ufugaji bora na kisa...
Picha
 

TVLA KUTOA HUDUMA YA CHANJO, KUPIMA MIFUGO BURE

Picha
Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania imepanga kutoa huduma ya Chanjo pamoja na upimaji wa magonjwa ya mifugo bure kwa maeneo yatakayobainishwa kwenye vituo vya 11 vilivyopo Tanzania nzima kuanzia tarehe 21/11/2022 hadi tarehe 25/11/2022 ikiwa ni maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwake. Akizungumza na vyombo vya habari Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania-TVLA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Dkt.Qwari Bura kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TVLA Dkt. Stella Bitanyi siku ya tarehe 20/11/2022 mtaa wa Bomani Mkoani Iringa kwa ajili ya kuutambulisha Umma alisema kwamba wakala imepanga kuwafikia wafugaji na kurudisha kile ilichokipata kwa jamii ikiwa ni Maadhimisho ya Miaka 10 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012. Dkt. Bura alisema kwamba wakala ilizinduliwa rasmi tarehe 11 Julai, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi na hadi kufikia mwaka huu 2022 Wakala imetimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake kutokana na kuunganishwa kwa iliyokuwa Maabara Kuu ya Mifugo (CVL), Vituo vya Kanda vya Uc...