Nav bar

Ijumaa, 25 Novemba 2022

 


Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah (wa pili kutoka kulia, mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Wizara mbalimbali za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwenye mkutano wa siku mbili wa Makatibu Wakuu (Committee of Senior Officials) wa Jumuiya ya IORA  unaofanyika Jijini Dhaka, Bangladesh kuanzia Novemba 22-23, 2022. Dkt. Tamatamah ameongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo ambao unatarajiwa  kuhitimishwa na kikao cha Baraza la Mawaziri kitakachofanyika Novemba 24, 2022. Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Baraza la Mawaziri utaongozwa na Mhe. Suleiman Masoud Makame, Waziri wa Uchumi wa Buluu na  Uvuvi wa SMZ.


Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah akitoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya hoja zilizojitokeza kuhusu Tanzania kwenye mkutano wa siku mbili wa Makatibu Wakuu (Committee of Senior Officials) wa Jumuiya ya IORA  unaofanyika Jijini Dhaka, Bangladesh kuanzia Novemba 22-23, 2022. Dkt. Tamatamah anaongoza ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo ambao unatarajiwa  kuhitimishwa na kikao cha Baraza la Mawaziri kitakachofanyika Novemba 24, 2022. Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Baraza la Mawaziri utaongozwa na Mhe. Suleiman Masoud Makame, Waziri wa Uchumi wa Buluu na  Uvuvi wa SMZ.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni