Nav bar

Ijumaa, 25 Novemba 2022

TVLA KANDA YA KATI YATOA ELIMU YA KWA WAFUGAJI

 


Meneja Wakala ya Maabara ya Mifugo Tanzania ( TVLA ) kanda ya kati Dodoma Dkt.Japhet Joas Nkangaga akiwa ofisini kwake Dodoma ameleza ratiba watakavyo tekeleza utoaji elimu kwa wafugaji katika maadhimisho ya wiki TVLA ni pamoja na kesho tarehe 22.11.2022 wataenda kutoa elimu  Halmashauri ya Dodoma vijijini,shule ya Amani,Mlezi na Kilimani.Tarehe 23.11.2022 timu ya wataalam itakuwa Hamashauri ya Bahi kuchanja Mifugo ya wafugaji na 24.11.2022 timu hiyo ya wataalam itakuwa Dodoma Jiji kuchukua sampuli ili kuchunguza magonjwa mbalimbali CBPP na kuchanja kuku dhidi ya ugonjwa wa Kideri. (21.11.2022)


Baadhi ya Wataalam wa TVLA Kanda ya kati wakiongozwa na Dkt.Harrison Gabriel  kushoto wakiwa na mteja wao ambaye amekuja kupa huduma ya elimu ya uchanjaji kuku dhidi ya kideri cha kuku leo katika ofisi za TVLA Kanda ya kati.Kauli Mbiu ya Maadhimisho hayo ni,"Tambua,Tibu na Udhibiti wa magonjwa ya Mifugo".( 21.11.2022 )


Maadhimisho ya wiki ya TVLA Kanda ya kati yameanza leo.ambapo maadhimisho hayo yanafanyika kwa kutoa huduma mbalimbali  kwa kufanfanya shughuli mbalimbLi za za kutoa huduma za afya ya  Mifugo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wafugaji wanaozunguka Mkoa huo.baadhi shughuli zinazofanyika ni pamoja na kutoa elimu ya udhibiti wa magonjwa,kutibu magonjwa na kutafiti vyakula vya Mifugo.kwa wafugaji wa mkoa wa Dodoma na vitongoji vyake.(21.11.2022).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni