Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Prof. Hezron Nonga akitoa neno la utangulizi wakati wa Kongamano la pili la Kitaifa la wadau la kujadili namna ya pamoja ya kuzuia usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 22-23, 2022. Kongamano hilo ni miongoni mwa matukio ya Wiki ya kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu usugu wa vimelea dhidi ya dawa iliyoanza Novemba 18-23, 2022. Kongamano hilo limeandaliwa na Wizara ya Afya, Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Vyuo Vikuu, Taasisi za Utafiti na Wadau wa Maendeleo.
Sehemu ya Wadau wa Kongamano la Kitaifa la kujadili namna ya pamoja ya kuzuia usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa wakifuatilia matukio mbalimbali yanayoendelea katika kongamano hilo linalofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 22-23, 2022.
Pichani ni muonekano wa sehemu ya ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania ambapo Kongamano la pili la Kitaifa la wadau la kujadili namna ya pamoja ya kuzuia usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa linapofanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 22-23, 2022.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni