Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Kanda ya Kati Dkt. Japhet Nkagaga wa (kwanza kulia) mwenye boksi la plastiki la kuhifadhia chanjo za mifugo, akitoa chanjo kwa ajili ya kuchanja Mifugo na pia ametoa elimu kwa moja ya Kikundi cha wafugaji wa kuku katika Kijiji cha Ilindi Wilayani Bahia,ambapo amewataka wafugaji hao kuona umuhimu wa kuchanja kuku kutumia chanjo ya I-2 dhidi ya ugonjwa Kideri ili kuwanusuru na vifo vya kuku wao katika Kikundi chao,ambapo ugonjwa huo ukiingia katika kaya ya mmoja wenu unauawa kuku takriban wote katika kaya.Lengo la kutoa elimu hii ni utaratibu wa Wakala ya Maabara ya veterinari kanda ya Kati waliojiwekea wa kutoa huduma ya afya ya Mifugo kwa wafugaji kanda hiyo katika kuadhimisha Wiki ya Wakala ya Maabara ya Veterinari kanda ya Kati Dodoma.(23.11.2022).
Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Kanda ya Kati Dodoma Dkt.Japhet Nkagaga akichanja Ng'ombe katika Kijiji cha Ilindi Kata ya Ilindi Wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma zaidi ya ng'ombe 350 wamechanjwa katika zoezi hilo katika Kata ya Ilindi dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Mapafu ya Ng'ombe (CBPP) ambao unaua Mifugo katika wilaya ya Bahi na hata Dodoma kwa ujumla wake. (23.11.2022)
Meneja wa Wakala ya Maabara ya Veterinari Kanda ya Kati Dodoma Dkt.Jophet Nkagaga mwenye Overoll la blue ( kushoto ) akitoa elimu katika Kijiji cha Ilindi Wilayani Bahi Mkoani Dodoma kuhusu umuhimu wa kudhibiti magonjwa Mifugo kwa kuchanja dhidi ya magonjwa hatari kwa kuuwa Mifugo hususan Ng'ombe,Mbuzi ,Mbwa na paka alitaja baadhi ya magonjwa hayo kuwa ni Homa ya mapafu ya ng'ombe (CBPP), Homa ya Mapafu Mbuzi ( CCPP), Miguu na Midomo,(FMD),Kutupa Mimba,Kichaa cha Mbwa ni lazima kuchanja dhidi ya magonjwa haya ili kuepuka hasara atayopata mfugaji endapo ng'ombe ataugua na kufa. Lengo la elimu hii ni utaratibu wa kanda kuhakikisha wafugaji wanapata huduma mbalimbali za za afya ya mifugo katika kipindi cha maadhimisho ya Wiki ya wakala ya Maabara ya Veterinari Kanda ya Kati Dodoma kuanzia tarehe 21 hadi 25.11.2022 huduma hizo ni Kuchanja,Kutibu, kuogesha,kuandaa vyakula vya Mifugo.(23.11.2022)
Mfugaji wa Kuku wa kienye katika Kijiji cha Ilindi, mwenye flana ya njano ambaye pia ni mwna kikundi cha umoja cha wafugaji wa kuku hao bw.John Lusinde anachanja kuku baada ya kupata elimu ya kuchanja kuku dhidi ya ugonjwa wa Kideri, hivyo atakuwa mwalimu wa wafugaji wengine kijijini na atakuwa akiwachanjia kuku katika kikudi hicho ambapo. Matumizi ya Chanjo ya I - 2 ni kuweka matone 2 ya chanjo ya l - 2 katika jicho la kuku chanjo hiyo itarudiwa baada ya miezi mitatu.(23.11.2022)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni