LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi inatarajia kuanza kutumia mfumo wa usimamizi wa utoaji vibali mbalimbali vya kusafirisha mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchi unaojulikana kama “ Mifugo Management Information System (MIMIS)” ambao unalenga kuboresha mazingira ya ufanyaji wa biashara za Mifugo, kukata na kuhuisha leseni za wataalam wa Mifugo na vibali vinavyohusu uingizaji, uzalishaji na uuzaji wa vyakula vya samaki. Hayo yamebainishwa leo na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia sekta ya Mifugo Dkt. Charles Mhina alipokuwa akifungua mafunzo ya matumizi ya mfumo huo kwa wadau na wataalam kutoka sekta za Mifugo na Uvuvi yaliyofanyika leo (18.05.2022) kwenye hoteli ya Royal Village jijini Dodoma. “Uwepo wa mfumo huu utatusaidia kuokoa muda wa kushughulikia vibali lakini pia utaongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kuokoa fedha za Serikali kwa sababu “Control Number” itazalishwa pale mtu anapofanya maombi tofauti na sasa ambapo mtu a...

Maoni
Chapisha Maoni