SERIKALI KUIMARISHA MIFUMO YA TAARIFA ZA MIKOPO KWA VIJANA
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, amesema serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi itaimarisha mifumo ya taarifa na takwimu kuhusu mikopo na uwezeshaji wa vijana kiuchumi ili kuongeza usimamizi wa miradi hiyo na kuhakikisha inakuwa na tija iliyokusudiwa. Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema hayo leo, Agosti 17, 2026, mara baada ya kuwasili mkoani Kagera akitokea jijini Mwanza, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua miradi na shughuli zinazotekelezwa na serikali, ikiwemo sekta ya mifugo na uvuvi. Akiwa Kagera, amekutana na Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mhe. Erasto Sima, na kufanya naye mazungumzo yanayolenga kuendeleza sekta za uvuvi na mifugo. Katika mazungumzo hayo, amesema mfumo mzuri wa taarifa na takwimu za utoaji wa mikopo kwa vijana utasaidia kuwa na usimamizi mzuri wa miradi ya uwezeshaji, lakini pia utaondoa upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya watu wenye nia ovu, hivyo akatoa rai kwa viongozi wa mikoa, wilaya...