DKT. BASHIRU: MIMI SITISHWI, NIACHENI NIFANYE KAZI YA RAIS ALIYONIPA

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amewaonya wanasiasa na baadhi ya watu wanaoendelea kujihusisha na kuhamasisha uvuvi usiofuata sheria maarufu kama uvuvi harama na kueleza kuwa ataendelea kuwa mstari wa mbele katika kulinda na kusimamia rasilimali za uvuvi nchini kwa maslahi ya taifa.

Kauli hiyo ameitoa Agosti 15, 2026 baada kuwatembelea wawekezaji wa viwanda vya kuchakata samaki jijini Mwanza na kuelezwa changamoto ya ukosefu wa malighafi za viwandani unaotoka na upungufu wa samaki Ziwa Victoria.

Mhe. Balozi Dkt. Bashiru amesema changamoto ya ukosefu wa malighali katika viwanda vya samaki imesababishwa na uvuvi usiofuata sheria katika maziwa hususan Ziwa Victoria, nakueleza kwamba Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia kikosi maalum alichokiunda kimeendelea kutoa elimu kwa vitendo pamoja na kufanya utafiti kuhusu chanzo cha vitendo hivyo ambapo katika hatua za awali kimebaini kuwa kuna watu ambao wamekuwa wakijihusisha na uvuvi haramu kutokana na baadhi ya wanasiasa kuwakingia mgongo .

"Tumekubaliana na mwekezaji tutatue tatizo la malighali na hali ni mbaya sana, nilivyojaribisha kidogo kutengeneza kikosi  kwa msaada wa Mheshimiwa Rais ambacho kitapita kutoa elimu kwa vitendo na kufanya utafiti wa vyanzo na mizizi ya tatizo hili, kwa hiyo niwatahadharishe waliozoea na ninawajua wote  kwa majina, wengine wanajifanya wanauswahiba na viongozi wa kisiasa, sitishwi, niacheni nifanye kazi ya mheshimiwa Rais" amesema Mhe. Balozi Dkt. Bashiru.

Ameongeza kuwa licha ya juhudi anazozifanya za kupambana na uvuvi haramu lakini bado kuna baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitetea vitendo vya uvuvi usiofuata sheria na akaeleza juu hatua iliyofikiwa  ya kukamilisha kanuni itakadhibiti uvuvi wa samaki walio chini ya kiwango ambapo Wizara ya Mifugo na Uvuvi Itasimamia na kulikomesha tatizo hilo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kiwanda cha Samaki cha Lake Star Company Bw. Peter Louis amesema hali mtikisiko wa kiuchumi duniani ulitokana vita vya mataifa makubwa imeathiri uendesheshaji wa viwanda kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa zinazotumika viwandani lakini pia suala la ukosefu wa malighali hususan samaki nalo bado changamoto kubwa katika uzalishaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Samaki cha Lake Star Company Limited Bw. Peter Louis akitoa maelezo kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kuhusu uchakataji wa samaki kiwandani hapo alipofanya ziara kukagua shughuli za uchakati wa samaki Agosti 15, 2026.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akikagua miundombinu ya kufugia samaki katika Shamba la Rofi Farm wakati wa ziara yake Wilayani Magu, Agosti 15, 2026.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (wa pili kulia), akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Magu Mhe. Jubilate Lawuo (wakwanza kushoto) na baadhi ya wataalam wa uvuvi kutoka wizarani kukagua samaki waliovuliwa kwenye Mradi wa Ufugaji Samaki TanGreen Wilayani Magu wakati wa ziara yake mkoani Mwanza Agosti 15, 2026.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TANZANIA DAIRY BOARD

SHAMBA LA KITULO KUWA KITOVU CHA NG’OMBE BORA WA MAZIWA NCHINI

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI