SERIKALI KUJENGA SOKO LA SAMAKI MCHINGA KWA MWAKA WA FEDHA 2026/2027
Serikali kuanza kutekeleza ahadi ya ujenzi wa Mwalo na Soko la Samaki katika Jimbo la Mchinga, mkoani Lindi, katika mwaka wa fedha 2026/2027, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha miundombinu ya sekta ya uvuvi nchini. Akijibu swali leo Novemba 2, 2026 Bungeni Jijini Dodoma, swali la Mbunge wa Mchinga, Mheshimiwa Salma Rashid Kikwete, aliyetaka kujua ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya ujenzi wa soko hilo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng’wasi Damas Kamani amesema Serikali tayari imefanya tathmini na kuthibitisha maeneo yatakayotumika kujenga miundombinu mipya ya uvuvi katika ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi. Aidha, Mhe. Kamani ameeleza kuwa katika Mwalo wa Mchinga, tathmini ya athari za kimazingira na kijamii tayari imekamilika, sambamba na michoro ya mradi, hatua zinazoweka msingi wa utekelezaji wa ujenzi huo, na ameongeza kuwa Serikali pia itajenga mialo na masoko ya uvuvi katika maeneo ya Kilwa-Kivinje, Shuka, Miseti na Kisiju, pamoja na kuboresha Soko la Samaki Bagamoy...