WIZARA NA BENKI KUU YAIKUTANISHA KAMPUNI YA CHOBO NA TAASISI ZA FEDHA

Wizara ya Mifugo na Uvuvi Kwa kushirikiana na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Oktoba 29, 2026 imefanya kikao na Benki za CRDB,TADB na Equity kujadili mgogoro wa muda mrefu na Kampuni ya Chobo Investments  kuhusu mikopo iliyochukuliwa na kampuni hiyo na dhamana yake.

Katika kikao hicho kilichofanyika Ofisi za Wizara zilizipo Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma, kilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Masoko, Bw. Stephen Michael, akiiwakilisha wizara katika, huku taasisi zingine zilizoshiriki ni pamoja na Benki Kuu ya Tanzania, Msajili wa Bodi ya Nyama Tanzania, Mkurugenzi wa Kampuni ya Ranchi za Taifa, Benki za CRDB, TADB, EQUITY na Kampuni ya Chobo Investiment Limited.

Kampuni hiyo kupitia kwa Mkurugenzi wake ilieleza kuwa mwaka 2014/15 ilichukua Mkopo katika Benki ya Equity wenye thamani ya shilingi bilioni 4.8, hata hivyo mkopo huo haukuiwezesha kampuni kuanza uzalishaji hivyo kushindwa kurejesha hadi deni hilo likakua kufikia Bilioni 10.5.

Pia, Chobo Investments iliwasilisha changamoto hiyo kwa BOT ili kuweza kusamehewa sehemu ya riba Kwa kuwa bado hajaanza uzalishaji ambapo mwisho wa majadiliano hayo, Benki ya Equity ilipunguza sehemu ya riba na deni halisi kufikia bilioni 8.5.

Kwa upande mwingine Benki za CRDB na TADB zilikubali kuingia kwenye mradi wa Chobo Investments ambapo TADB ilikubali kurithi deni la bilioni 7.3 na CRDB bilioni 1.2, hata hivyo wakati Benki zinataka zianze kurejesha fedha hizo Kwa Benki ya Equity, ambayo imesema hadi sasa deni lake la bilioni 1.2 limekuwa hadi kufikia bilioni 3.9.

Baada ya mazungumzo yote hayo, Benki Kuu iliielekeza Kampuni ya Chobo Investment iwasilishe barua kwenda Equity kupitia Benki ya CRDB kuwa imekusudia kulipa Bilioni 1.2 ambayo Kampuni hiyo inadaiwa na baada ya hapo,mijadala itaanza ya kutatua changamoto hiyo.







Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TANZANIA DAIRY BOARD

SHAMBA LA KITULO KUWA KITOVU CHA NG’OMBE BORA WA MAZIWA NCHINI

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI