DKT. KIULA AWASILI RASMI TAFICO, AHIMIZA UWAJIBIKAJI NA UBUNIFU

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), Dkt. Suleiman Peter Kiula, ndc, leo Agosti 14, 2026, amewasili rasmi ofisi za Makao Makuu ya Shirika zilizopo Kigamboni Dar es Salaam, na kuzungumza na watumishi wa Shirika, akisisitiza umuhimu wa mshikamano, nidhamu na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya TAFICO.

Dkt. Kiula amesema TAFICO ina majukumu makubwa katika mnyororo wa thamani wa sekta ya uvuvi, ikiwemo uendeshaji wa meli, bandari, viwanda vya uchakataji wa mazao ya uvuvi pamoja na kuingia katika ufugaji wa samaki. 

Katika kuyafanikisha malengo ya Shirika, Dkt. Kiula ametoa rai kwa watumishi kuwa sehemu ya Shirika na kila mmoja kuwa kiongozi katika eneo lake la utendaji, huku akisisitiza nidhamu na ushirikiano.

“Tutasimama pamoja, tutashirikiana ili tutengeneze historia ya sekta ya uvuvi nchini. TAFICO inaanza safari ya kwenda kuingia bahari kuu.” alisisitiza.

Afisa Mtendaji Mkuu  wa Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO), Dkt. Suleiman Peter Kiula, ndc, (kushoto) akikabidhiwa nyaraka za utendaji kazi na aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TAFICO CPA Shaibu Matessa, kama ishara ya kukabidhiwa ofisi rasmi  leo Agosti 14, 2026, katika ofisi za Makao Makuu ya Shirika zilizopo Kigamboni Dar es Salaam.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TANZANIA DAIRY BOARD

SHAMBA LA KITULO KUWA KITOVU CHA NG’OMBE BORA WA MAZIWA NCHINI

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI