WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI YATOSHANA NGUVU NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS
◾Yatoa sare ya 1-1, huku Rogers Charles akiibuka Mchezaji Bora wa Mechi.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Ofisi ya Makamu wa Rais katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo, Agosti 14, 2026, katika Viwanja vya Kilimani, Dodoma.
Mchezo huo ni sehemu ya maandalizi kuelekea Mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI).
Ofisi ya Makamu wa Rais ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 54 kupitia mchezaji wake, Rashid Mzee, aliyefanikiwa kuipatia timu yake uongozi.
Hata hivyo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi haikukata tamaa, na juhudi zake zilizaa matunda baada ya kufanya mabadiliko ya mchezo na kumtoa Stanley Brayton dakika ya 60 na kuingia Mchezaji Rogers Charles, na hatimaye dakika ya 87 mchezaji Rogers Charles akafunga bao la kusawazisha kwa njia ya mpira wa adhabu na kuifanya mechi kumalizika kwa sare ya 1-1.
Rogers Charles aliibuka kuwa Mchezaji Bora wa Mechi, baada ya kuonyesha kiwango kizuri na kufunga bao muhimu lililoipa timu yake sare katika dakika za mwisho za mchezo.
Matokeo hayo yanaendelea kutoa nafasi kwa timu zote mbili kujiimarisha zaidi katika maandalizi yao kuelekea mashindano ya SHIMIWI.

Maoni
Chapisha Maoni