Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2021

MBEYA KUTENGA BAJETI YA UNYWAJI MAZIWA SHULENI

Picha
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote zilizopo mkoani kwake kutenga bajeti ya maziwa kwa wanafunzi wote wa shule za awali na msingi waliopo mkoani humo. Homera ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kilele cha Siku ya unywaji maziwa shuleni ulimwenguni ambayo kitaifa imefanyika leo (29.09.2021) mkoani Mbeya amesema kuwa suala la unywaji maziwa shuleni kwa wanafunzi ni la lazima na si hiyari. “Hatuwezi kusubiri wadau tu kila siku wajitoa wakati watoto ni wetu wenyewe hivyo ni lazima wakati wa kupanga bajeti zote za halmashauri zilizopo mkoani Mbeya iwekwe bajeti ya kutekeleza mpango huu na kwa sababu mimi ndo naidhinisha bajeti zote,sitopitisha bajeti yoyote ambayo haina bajeti ya kutekeleza mpango huo” Amesema Homera. Aidha Homera amepongeza juhudi na kazi inayofanywa na Wizara ya mifugo na Uvuvi kupitia bodi ya maziwa kwa kuwa karibu na wadau mbalimbali wa tasnia ya maziwa waliopo mkoani humo ambapo amewataka wasindikaji wote wa maziwa nchini k...

MKANDARASI ATAKIWA KUFUATA TARATIBU NA KANUNI UJENZI WA MAJENGO YA MIHADHARA.

Picha
Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) Dkt. Pius Mwambene ametaka ujenzi wa vyumba viwili vya mihadhara katika chuo hicho Tawi la Tengeru Mkoani Arusha kujengwa kwa kufuata taratibu na kanuni za ujenzi. Dkt. Mwambene amebainisha hayo katika ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo katika jengo la NBC jijini Dodoma, wakati wa utiaji saini wa ujenzi wa vyumba hivyo. Alisema anatarajia kazi ya ujenzi itatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya ubora na kukamilika kwa wakati uliopangwa. Aliongeza kuwa mkataba unaonyesha muda wa ujenzi  uliopangwa ni miezi sita, ambapo ujenzi utaanza mwishoni mwa mwezi huu wa Septemba na kukamilika  mwishoni mwa mwezi wa Machi mwaka 2022. Aidha Mtendaji huyo alisema kuwa gharama za ujenzi wa vyumba viwili vya mihadhara ni Shilingi Milioni 800 hadi utakapokamilika. Awali akiongea baada ya zoezi la utiaji saini kukamilika Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Ugani na Mafunzo Dkt. Angelo Mwilawa ameitaka kampuni ya...

ZIWA VICTORIA KUFANYIWA MPANGO BORA WA MATUMIZI KUKUZA UCHUMI WA BULUU

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kufanya mpango wa matumizi bora ya ziwa Victoria ambao utaainisha maeneo ambayo yatatumika kufanya ufugaji wa vizimba ili kutoa nafasi pia kwa shughuli za uvuvi wa asili kuendelea bila kuwa na muingiliano. Ulega aliyasema hayo Septemba 27, 2021 alipotembelea eneo la Kampuni ya Kichina ya Tangreen iliyowekeza katika mradi wa ufugaji wa Samaki kwa kutumika vizimba kandokando ya ziwa Victoria, jijini Mwanza. Alisema kuwa serikali imedhamiria kufanya hivyo ili kupunguza muingiliano wa shughuli za ufugaji wa Samaki na Uvuvi wa asili ili shughuli zote zifanyike kwa ufanisi na kuleta tija katika uchumi wa buluu. "Mpango wa Serikali ni kuhakikisha ufugaji wa vizimba unafanyika katika maeneo maalum na sio kila mahala, tuwe na maeneo mahsusi ya kazi hii ili kutoa nafasi pia wavuvi wa asili waweze kuendelea na shughuli zao," alisema Ulega Wa...

SERIKALI YADHAMIRIA KUBORESHA BIASHARA YA MIFUGO NCHINI.

Picha
  Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuboresha mazingira ya biashara ya mifugo, ikiwemo ujenzi wa mnada wa upili wa nyamatala ili kuendelea kuchochea uchumi wa taifa. Hayo yalisemwa   na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Amosy Zephania, wakati akizungumza na wafanyabiashara wa mifugo wa mnada wa upili Nyamatala uliopo Wilayani Misungwi mkoani Mwanza Septemba 27,2021. Alisema Wizara ya Mifugo na Uvuvi itaendelea kuhamasisha wafanyabiashara wa mifugo kukutana na wenye viwanda, wazungumze na kukubaliana bei ili kuwezesha upatikanaji wa mifugo yenye ubora ambao unahitajika kwenye viwanda na wafanyabiashara hao kupata soko zaidi. "Lengo ni kuendelea kuona mifugo inapata thamani, ambapo watu wa viwandani wanadai kuwa mifugo wanayopelekewa haina ubora wanao wanaouhitaji." Alisema Aliongeza kuwa wanaposema biashara, wanaanzia sokoni, Wizara pamoja na serikali kwa u...

ULEGA AINGILIA KATI MGOGORO SHAMBA LA SERIKALI NANGARAMO NA WANANCHI

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu kuweka utaratibu mzuri wa kugawa kwa muda sehemu ya shamba la kuendeleza Mifugo la Nangaramo na kuwapatia wananchi wanaoishi karibu na shamba hilo ili waweze kufanya shughuli zao za kilimo. Ulega alitoa maelekezo hayo Septemba 24, 2021 kufuatia malalamiko aliyoyapata kutoka kwa wananchi wanaoishi karibu na shamba hilo kukosa maeneo ya kulima wakidai kuwa mipaka ya shamba hilo imewekwa ndani ya maeneo yao ya asili ya kilimo. Akiwa katika shamba hilo lililopo Wilayani Nanyumbu, Mkoani Mtwara, Naibu Waziri Ulega alipata fursa ya kusikiliza kero za wananchi hao ambao wengi wao waliiomba Serikali kuwapatia sehemu ya eneo la shamba hilo ili waweze kulima zao la mpunga. Baada ya kusikiliza malalamiko ya Wakulima hao ambao walisema maeneo yao yamechukuliwa na shamba hilo, Ulega alimuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo kupitia upya maeneo ya mipaka ya shamba hilo ili waone ni sehemu gani katika shamba hilo wanaw...

SERIKALI KUFANYA MAPITIO SHERIA NA KANUNI SEKTA YA UVUVI NCHINI

Picha
Serikali ipo katika mchakato wa kufanya mapitio ya sheria na kanuni zinazo simamia sekta ya uvuvi nchini ili kukuza na kuendeleza viumbe maji ikiwemo ufugaji samaki kwa kutumia vizimba. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe.Mashimba Ndaki amebainisha hayo   September 24,2021 jijini Dodoma wakati alipozungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushiriki mkutano wa kimataifa wa kukuza na kuendeleza ukuzaji viumbe maji ulifanyika kwa njia ya video. Mashimba, alisema lengo la kupitia sheria pamoja na kanuni katika sekta hiyo ni kuhakikisha kuwa zinawezesha uvuvi wa kutumia vizimba pamoja na mabwawa. “Sheria pamoja na kanuni zetu awali sekta hii ya uvuvi ilikuwa imemezwa na uvuvi wa majini tuu hivyo tunafanya mapitio ili kuwezesha uvuvi huu wa kutumia vizimba unakuwa na mchango katika kuongeza pato la taifa” alisema Mashimba. Akizungumzia mkutano huo alisema lengo lake ni kuwezesha nchi washiriki kukuza na kuendeleza ukuzaji wa viumbe maji kwa kutumia uvuvi wa vizimba, mabwawa pam...

WAZIRI NDAKI ATEKELEZA AGIZO LA RAIS, AGAWA ENEO KWA WAFUGAJI

Picha
  Serikali imekabidhi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza eneo lenye ukubwa wa Hekta 6,000 lililotolewa kwa wananchi wa vijiji vya Mpeta na Chakuru ili ligawiwe kwa wananchi hao kwa ajili ya shughuli za ufugaji baada ya mgogoro wa muda mrefu wa wananchi hao kuvamia Hifadhi ya Ranchi ya Taifa ya Uvinza iliyopo Mkoani Kigoma. Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Mashimba Ndaki amekabidhi eneo hilo (23.09.2021), akitekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ameamua eneo hilo kumegwa kutoka Hifadhi ya Ranchi ya Taifa ya Uvinza baada ya kusikia kilio cha wafugaji hao kutoka mikoa ya kanda ya ziwa kutokuwa na maeneo kwa ajili ya mifugo yao. Waziri Ndaki alibainisha kuwa hatua hiyo inakuja kukiwa na mgogoro mkubwa baina ya wananchi hao ambao ni wafugaji, Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza na Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) ambapo wananchi zaidi ya 5,900 wamevamia eneo la ranchi hiyo kitongoji cha Mwanduhubanhu kijiji cha Mpeta na eneo la Kaza...

ULEGA: TUMEDHAMIRIA KUWAWEZESHA WAVUVI WAONDOKANE NA UVUVI WA KUWINDA

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imepanga kuwaelimisha Wavuvi na kuwapa vifaa maalum vitakavyowasaidia kujua wapi kuna makundi ya Samaki ili waachane na Uvuvi wa kuwinda ambao umekuwa hauna tija kwao. Ulega aliyasema hayo katika hafla fupi ya kuwakabidhi Wavuvi na Wakulima wa Mwani vifaa vya kufanyika kazi vikiwemo injini ya boti na Kamba za kulimia zao la Mwani iliyofanyika katika Kijiji cha Mchinga, Mkoani Lindi Septemba 23, 2021. "Sasa hivi tunatumia njia ya 'Satelite' kujua mavuvi yetu yako wapi, samaki wako wapi, kifaa cha GPS kinamsaidia mvuvi kabla hajatoka Pwani kujua aende umbali gani ambako kuna makundi ya Samaki,"alisema Ulega Aidha, alitumia nafasi hiyo kuwataka Wavuvi na Wakulima wa zao la Mwani kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwaletea maendeleo. Katika hafla hiyo, Naibu Waziri Ulega aliwapatia Wavuvi injini moja ya boti yenye thamani ya S...

SERIKALI YA RAIS SAMIA KUWAINUA KIUCHUMI WANANCHI WA RUANGWA

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kupeleka miradi ya ufugaji Kuku, Mbuzi na  Samaki katika Wilaya ya Ruangwa ili iwasaidie  kuinua Uchumi wao. Ulega aliyasema hayo  wakati akiongea na Viongozi wa Wilaya ya Ruangwa iliyopo Mkoani Lindi  Septemba 22, 2021. Alisema kutokana na kasi kubwa ya maendeleo ya Wilaya hiyo inayochochewa na shughuli za uchimbaji madini Serikali imeona ni vyema kupeleka miradi hiyo kwa kina mama na vijana ili kukuza uchumi wao na kukidhi mahitaji ya mazao ya Mifugo katika Wilaya hiyo. Naibu Waziri Ulega aliitaja miradi hiyo ambayo  itapelekwa katika Wilaya hiyo na kuwasaidia wakina mama na vijana ni pamoja  ufugaji wa kuku na ufugaji wa Samaki na Mradi wa Kopa mbuzi lipa mbuzi. "Mwezi Oktoba tutaanza na Vikundi kumi, tutaleta Wilayani hapa kuku elfu mbili (2000) ikiambatana na semina ya kuelekeza namna ya kufuga kuku hao kibiashara," alisema Ulega...

NACHINGWEA YATAKIWA KUSIMAMIA MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Hashim Komba kuhakikisha anawapanga Wakulima na Wafugaji katika maeneo waliyopangiwa ili kuondosha migogoro inayoikabili Wilaya hiyo. Ulega aliyasema hayo wakati akiongea na Wakulima na Wafugaji wa Kata za Matekwe, Kilimarondo, Kiegei na Mbondo alipofanya ziara katika Wilaya hiyo ya Nachingwea, Mkoani Lindi kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za Wakulima na Wafugaji Septemba 21, 2021. Alisema kuwa ili Wilaya hiyo iondokane na migogoro ya Wakulima na Wafugaji ni lazima Serikali isimamie mpango wa matumizi bora ya ardhi ambao tayari wanao. "Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya mfugaji au mkulima anayefanya shughuli katika eneo ambalo hakupangiwa mtoe mpeleke katika eneo analopaswa kufanya shughuli zake, ni lazima tusimamie utaratibu tuliojiwekea kwa mujibu wa sheria," alisema Ulega kuhusu tatizo la maji ya kunyweshea Mifugo linalowasumbua Wafugaji wa maeneo hayo, Ulega alisema kuwa Rais ...

SERIKALI KUENDELEA KUHAMASISHA ULAJI WA NYAMA NCHINI.

Picha
  Wizara ya Mifugo na Uvuvi   imesema  bado ulaji wa nyama nchini Tanzania  ni mdogo ambapo kwa sasa ulaji ni kilo 15 kwa mtu tofauti na tafiti za shirika la chakula Duniani  linaloelekeza kila mtu atumie kilo 50 kwa mwaka.  Akizungumza,  Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Amosy Zephania  katika ziara yake ya kikazi  katika  shamba la kuku la Irvine  wilayani siha Mkoani Kilimanjaro Septemba 21,2021 ambapo  alisema kuwa  kutokana na hali hiyo serikali inatarajia kuendelea kutoa elimu kwa watanzania kuona umuhimu wa ulaji wa nyama . “Sensa ya mifugo ya mwaka 2019/2020 inanyesha katika kaya zinazijishughulisha na kilimo na ufugaji  Tanzania ni zaidi ya milioni saba, kaya zaidi ya milioni nne sawa na asilimia 55. 3 wanafuga kuku kuanzia 10 na kuendelea, hii inaonyesha jinsi tunavyozungumza kuku tu, nazungumzia maisha ya watanzania kwanzia ngazi ya chini  hadi juu, "amesema  Alisema ni...

SERIKALI KUJENGA BWAWA LA MIL. 480 LIWALE

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema katika bajeti ya mwaka 2021/2022 Serikali itajenga bwawa la kunyweshea Mifugo lenye thamani ya Shilingi Milioni 480 katika Kijiji cha Kimambi, Wilayani Liwale, Mkoani Lindi. Ulega aliyasema hayo Septemba 20, 2021 alipofanya ziara katika Wilaya ya Liwale, Mkoani Lindi kwa lengo la kusikiliza kero za Wafugaji na Wakulima ili kuzitatua. Alisema ujenzi wa bwawa hilo utasaidia kutatua changamoto ya maji ambayo inawakabili wafugaji wa maeneo hayo na utasaidia pia kutatua migogoro baina yao na wakulima Wilayani humo. "Rais Samia Suluhu Hassan anakwenda kuwajengea bwawa lenye thamani ya Shilingi Milioni 480 hapa Kimambi, ujenzi wa bwawa hilo utasaidia kuwaondosha katika migogoro," alisema Ulega Naibu Waziri Ulega alisisitiza kuwa  pesa hizo zipelekwe kufanya kazi iliyopangiwa ya ujenzi wa bwawa la kunyweshea mifugo huku akiwataka viongozi wa Wilaya hiyo kuhakikisha pesa hizo zinatumika vizuri. Aidha, alisema kuwa Rai...

*ULEGA AWATAKA WAFUGAJI PWANI KUVUNA MIFUGO YAO*

Picha
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewataka Wafugaji wa Mkoa wa Pwani kuanza kuvuna Mifugo yao na kuiuza kwani kwa kufanya hivyo kutawasaidia kuwaongezea kipato na kupunguza migogoro kati yao na watumiaji wengine wa ardhi. Ulega aliyasema hayo Septemba 19, 2021 wakati akiongea na Wafugaji na Wakulima wa Wilaya ya Rufiji alipofanya ziara Wilayani humo ya kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi. Alisema ni muhimu viongozi wa Wilaya za Rufiji, Mkuranga na Kibiti kukaa na wadau wa mifugo kutengeneza mkakati wa kuhamasisha uvunaji wa mifugo yao kwakuwa soko la kuuza lipo mkoani humo na bado hawajalitumia ipasavyo. "Hapa Mkoa wa Pwani tuna Kiwanda cha Nyama cha TanChoice lakini pamoja na kiwanda hicho kuwepo hakuna mifugo inayopelekwa pale kutoka ukanda wetu huu wa Pwani," alisema Ulega Aliongeza kwa kusema kuwa ili faida ya uwepo wa kiwanda hicho ionekane ni vyema wadau wote wa mifugo mkoani humo waanze uvunaji mkubwa na kupeleka kuiuza kiwandani ha...