Naibu Waziri wa
Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Hashim
Komba kuhakikisha anawapanga Wakulima na Wafugaji katika maeneo waliyopangiwa
ili kuondosha migogoro inayoikabili Wilaya hiyo.
Ulega aliyasema
hayo wakati akiongea na Wakulima na Wafugaji wa Kata za Matekwe, Kilimarondo,
Kiegei na Mbondo alipofanya ziara katika Wilaya hiyo ya Nachingwea, Mkoani
Lindi kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za Wakulima na Wafugaji
Septemba 21, 2021.
Alisema kuwa
ili Wilaya hiyo iondokane na migogoro ya Wakulima na Wafugaji ni lazima
Serikali isimamie mpango wa matumizi bora ya ardhi ambao tayari wanao.
"Mheshimiwa
Mkuu wa Wilaya mfugaji au mkulima anayefanya shughuli katika eneo ambalo
hakupangiwa mtoe mpeleke katika eneo analopaswa kufanya shughuli zake, ni
lazima tusimamie utaratibu tuliojiwekea kwa mujibu wa sheria," alisema
Ulega
kuhusu tatizo
la maji ya kunyweshea Mifugo linalowasumbua Wafugaji wa maeneo hayo, Ulega
alisema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ametenga Shilingi Milioni 480 kwa ajili
ya kujenga Bwawa la kunyweshea Mifugo litakalojengwa katika Kijiji cha Matekwe
Kilichopo Wilayani humo ili Wafugaji wawe na maji ya uhakika wakati wa
kiangazi.
"Sio bwawa
tu, Rais Mama Samia atawajenge Josho kwa ajili ya kuogeshea mifugo, Milioni 18
zitatolewa kwa ajili ya kazi hiyo, Sasa nitashangaa sana nikiona wafugaji
mnaendelea kuzagaa," alisisitiza Ulega
Aidha, alitumia
fursa hiyo pia kuwaonya Wakulima na Wafugaji hao kuacha vitendo vya
kujichukulia Sheria mkononi kwani havifai na vinahatarisha amani katika jamii.
Naye Mkuu wa
Wilaya wa Nachingwea, Hashim Komba alimuhakikishia Naibu Waziri Ulega kuwa
maelekezo yote aliyoyatoa atayafanyia kazi na kisimamia sheria ili utaratibu
ufuatwe.
Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiongea na Wafugaji na Wakulima wa
Kata za Matekwe, Kilimarondo, Kiegei na Mbondo alipofanya ziara katika Wilaya
ya Nachingwea iliyopo Mkoani Lindi kwa lengo la kusikiliza na kutatua kero za
Wakulima na Wafugaji Septemba 21, 2021. Katika Mkutano huo Naibu Waziri
alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Hashim Komba (kushoto) kuhakikisha
anasimamia Mpango wa matumizi bora ya ardhi na kuwapanga Wafugaji na Wakulima
katika maeneo husika.
Sehemu ya Wafugaji na Wakulima waliohudhuria Mkutano wa Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (hayupo pichani) alipokuwa akiongea
nao katika Kijiji cha Kilimarondo, Wilayani Nachingwea, Mkoani Lindi Septemba
21, 2021.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni