Wizara ya Mifugo na Uvuvi imesema bado ulaji
wa nyama nchini Tanzania ni mdogo ambapo kwa sasa ulaji ni kilo 15 kwa
mtu tofauti na tafiti za shirika la chakula Duniani linaloelekeza kila
mtu atumie kilo 50 kwa mwaka.
Akizungumza, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi,
Bw. Amosy Zephania katika ziara yake ya kikazi katika shamba
la kuku la Irvine wilayani siha Mkoani Kilimanjaro Septemba 21,2021
ambapo alisema kuwa kutokana na hali hiyo serikali inatarajia
kuendelea kutoa elimu kwa watanzania kuona umuhimu wa ulaji wa nyama .
“Sensa ya mifugo ya mwaka 2019/2020 inanyesha katika kaya
zinazijishughulisha na kilimo na ufugaji Tanzania ni zaidi ya milioni
saba, kaya zaidi ya milioni nne sawa na asilimia 55. 3 wanafuga kuku kuanzia 10
na kuendelea, hii inaonyesha jinsi tunavyozungumza kuku tu, nazungumzia maisha
ya watanzania kwanzia ngazi ya chini hadi juu, "amesema
Alisema ni wajibu wa Kampuni hiyo kuhamasisha wananchi
kujikita katika ufugaji wa kuku hali itakayo peleka ongezeko la ulaji wa
nyama kwa watanzania.
" Toeni elimu kwa jamii, jitanganezi, zipo pesa katika kila
halmashauri nchi nzima fikeni huko, zungumzeni na wakurugenzi
wakopesheni kuku vijana, kinamama, watu wenye ulemavu, uwezo wa kulipa
upo, kwa kufanya hivyo tutawafikia watanzania wengi zaidi na ulaji wa nyama
utaongezeka, "amesema
Kwa upande wake meneja masoko na uendelezaji wa biashara wa
Kampuni hiyo nchini, Jeremia Kilato alisema wanazalisha vifaranga zaidi
laki 220 kwa wiki, ingawa wanatarajia kuongeza uzalishaji hadi kufikia zaidi ya
laki 290 kwa wiki.
" Tunajivunia uzalishaji wa kisasa na wenye ubora wa
kimataifa, lakini kwa sasa tunakabiliwa na changamoto, ni ongezeko kubwa la
uhitaji wa vifaranga hasa katika kipindi hichi cha Uviko 19, Kampuni
imeweka mikakati ya kuweza kununua mashine mpya
itakayoongeza uzalishaji kutoka 220 hadi 290,"amesema.
Alisema, wanatarajia kuendelea kusambaza vifaranga
katika Wilaya zote na Mikoa yote ambapo hadi sasa tayari
wamesambaza katika mikoa 13.
Kwa upande wake meneja wa kituo cha uwekezaji Kanda ya Kaskazini,
Bw. Daudi Riganda alisema mwekezaji huyo yupo kihalali na yupo kwenye hatua za
mwisho.
Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Amosy Zephania (waliokaa katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa shamba la irvine's wa pili kutoka kushoto ni Bw. Darryl Combe na wa pili kutoka kulia ni Bw. Fabio Stella pamoja na watumishi wa shamba hilo na watumishi kutoka Wizara ya Mifugo na uvuvi, mara baada ya kutembelea shamba hilo lililopo Siha Mkoani Kilimanjaro. Septemba 21,2021.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni