Serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuboresha mazingira ya
biashara ya mifugo, ikiwemo ujenzi wa mnada wa upili wa nyamatala ili
kuendelea kuchochea uchumi wa taifa.
Hayo yalisemwa na Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya
Mifugo na Uvuvi (Mifugo), Bw. Amosy Zephania, wakati akizungumza na
wafanyabiashara wa mifugo wa mnada wa upili Nyamatala uliopo Wilayani
Misungwi mkoani Mwanza Septemba 27,2021.
Alisema Wizara ya Mifugo na Uvuvi itaendelea kuhamasisha
wafanyabiashara wa mifugo kukutana na wenye viwanda, wazungumze na
kukubaliana bei ili kuwezesha upatikanaji wa mifugo yenye ubora ambao unahitajika kwenye
viwanda na wafanyabiashara hao kupata soko zaidi.
"Lengo ni kuendelea kuona mifugo inapata thamani,
ambapo watu wa viwandani wanadai kuwa mifugo wanayopelekewa haina ubora
wanao wanaouhitaji." Alisema
Aliongeza kuwa wanaposema biashara, wanaanzia sokoni, Wizara
pamoja na serikali kwa ujumla mpaka sasa ina viwanda vitano vikubwa
vinavyotegemea malighafi za mifugo ikiwemo kiwanda cha Chobo Misungwi na
Tan Choice.
"Sisi tumekuja kutoa rai kwenu, wenye viwanda waje
wazungumze na nyinyi, wawaeleze wanataka mifugo ya aina gani, mifugo
inenepeshwe kwa kiwango gani na watatoa bei gani, Alisema Bw. Zephania.
Mmoja wa wafanyabiashara wa mifugo mnada wa upili
Nyamatala Bw. Emmanuel Mgelwa, aliipongeza serikali kuwatimizia mahitaji
waliokuwa wanayataka katika mnada huo ila changamoto ni suala la ulinzi.
Naye Tabu Shindika, aliiomba serikali kuleta mnada wa mbuzi
katika eneo hilo ili mtu akitaka ng'ombe, mbuzi na kondoo wapate hapo
kwenye mnada wa Nyamatala.
Kaimu katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo),
Bw. Amosy Zephania akiongea na wafugaji pamoja na wafanyabiashara wa Mifugo
wa mnada wa Upili nyamatala wakati wa ziara yake Mkoani Mwanza. Lengo ni kujua
changamoto zinazowakabili katika biashara yao na kujadili njia Bora za kuweza
kutatua changamoto hizo kwenye mnada Huo Mkoani Mwanza. Septemba 27,2021
|
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni