SERIKALI KUENDELEA KUUNGANISHA NGUVU KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KWA MIFUGO
Serikali imesema itaendelea kuimarisha ushirikiano baina ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo na Wizara ya Maji ili kuhakikisha changamoto ya upatikanaji wa maji kwa mifugo inatatuliwa nchini, kauli ambayo imetolewa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Ng’wasi Damas Kamani wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kiteto, Mhe.Edward Kisau Olelekaita, aliyetaka kujua mkakati wa Serikali wa kuunganisha nguvu za wizara hizo katika kuboresha miundombinu ya maji katika Jimbo la Kiteto. Akijibu swali katika Kikao cha Bunge la kumi na tatu, mkutano wa tano, kikao cha sita, leo Novemba 3, 2026 Bungeni Jijini Dodoma, swali la Mhe. Olelekaita aliyetaka kujua ni lini Serikali itapeleka fedha za kukamilisha mradi wa bwawa la maji ya mifugo la Kiwani, lililopo Kata ya Ndeda, Wilaya ya Kiteto, Mhe. Kamani alisema Serikali inatambua umuhimu wa mradi huo katika kuboresha upatikanaji wa maji kwa mifugo na wananchi, na kwamba mradi huo utaendelea kuzingatiwa katika mipango ya bajeti ya...