Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2026

MAENDELEO YA UJENZI WA SOKO LA SAMAKI KIPUMBWI HAYARIDHISHI - PROF. SHEIKH

Picha
Na. Stanley Brayton  ◾Wizara yagoma kuzungumzia kuongeza Mkataba. ◾Awashauri wataalam wa Halmashauri kufuatililia kwa karibu Maendeleo ya Mradi. Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Prof. Mohammed Ali Sheikh amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya World Class Engineering Contractors Limited kumaliza Ujenzi wa Mradi wa soko la Samaki Kipumbwi haraka iwezekanavyo ili kuweza kuwapa nafasi wavuvi wanaotegemea Soko ilo katika kukuza vipato vyao kwa kufanya biashara, Mradi ambao unatekelezwa chini ya Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kilimo (IFAD). Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, katika ziara yake ya kikazi Mkoani Tanga na kukagua Maendeleo ya Miradi wa Soko la Samaki la Kipumbwi lililopo Wilayani Pangani, leo Februari 27, 2026, Prof. Sheikh amesema soko la Samaki la Kipumbwi ni tegemo kubwa sana kwa wavuvi na ni soko ambalo litasaidia kukuza Uchumi wa wananchi na wa Taifa kiujumla. "ni vy...

WAUZAJI VYAKULA VYA MIFUGO WATAKIWA KUSAJILI NA KUHUISHA VYETI VYAO VYA USAJILI

Picha
Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo Februari 27, 2026, imefanya ukaguzi wa maeneo ya kuuza, kuzalisha na kuhifadhi rasilimali za vyakula vya mifugo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma, kwa lengo la kuhakikisha vyakula vinavyozalishwa vinakuwa na ubora na wadau wanafata taratibu, miongozo, kanuni na sheria. Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Vyakula vya Mifugo, Bi Theodata Sallema, amesema pamoja na kukagua ubora wa vyakula vinavyozalishwa, Pia Wizara inaangalia kama wafanyabiashara wanafanya biashara kwa mujibu wa sheria, ikiwemo kusajili maeneo yao ya biashara. "Ukaguzi  huo, unalenga kubaini namna vyakula vinavyozalishwa,  kuhifadhiwa na kusambazwa ili kuhakikisha havileti madhara kwa mifugo wala kwa mlaji wa mazao yatokanayo na mifugo hiyo".Bi. Sallema Aidha, amebainisha kuwa Wizara inaendelea kuwasaidia wadau kujiunga kwenye mfumo wa utoaji vibali wa kielektroni yaani MIMIs, ili kurahisisha mchakato wa ma...

SERIKALI YAANZISHA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA UVUVI

Picha
Na. Stanley Brayton ◾Vizimba vya Bahari kuanza. ◾Wizara kuanzisha Mikakati ya Kimageuzi Sekta ya Uvuvi yatajwa. ◾ Vifaranga vya Samaki maji baridi na maji chumvi kupandikizwa. Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza utekelezaji wa Mpango Mkakati wa kufuga samaki kwa njia ya Vizimba katika bahari, mpango ambao utasaidia kuongeza Uzalishaji wa Samaki chumvi na Masoko nje ya nchi. Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Naibu Katibu Mkuu (Uvuvi), Prof. Mohammed Ali Sheikh, katika ziara yake ya kikazi Mkoani Tanga alipotembelea Kituo cha Ukuzaji Viumbemaji Machui kwa ajili ya kukagua Maendeleo ya Mradi wa kuzalisha chakula cha Samaki aina ya Viroboto maji (Atemia), leo Februari 27, 2026, amesema Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa sasa ipo katika utekelezaji wa kukuza Viumbemaji kwa njia ya Vizimba kupitia bahari, mpango ambao utaongeza tija katika Sekta ya Uvuvi. "Mpango huu ni mpango mzuri ambao utekelezaji wake unategemea kuanza kufanyika ndani ya miezi...

BI. MEENA AONGOZA KIKAO CHA MAGEUZI YA SEKTA YA MAZIWA

Picha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agness Meena, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utekelezaji wa Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi, leo Februari 27, 2026, jijini Dar es Salaam ameongoza kikao muhimu cha wajumbe wa kamati hiyo kutoka Tanzania Bara na Visiwani. Kikao hicho kililenga kupitia kwa pamoja hatua za utekelezaji wa mradi tangu kuanza kwake hadi sasa, pamoja na kujadili mikakati madhubuti ya kuendeleza utekelezaji wake kwa ufanisi zaidi. Bi Meena amesisitiza kwa wajumbe pamoja na sekretarieti ya kamati umuhimu wa kuwa na mgawanyo sahihi wa majukumu, ushirikiano wa karibu pamoja na mawasiliano yenye tija. Hatua hizi ni muhimu ili kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa wakati na kufikia malengo yaliyokusudiwa. Kwa upande wake, Mwenyekiti Mwenza wa kamati hiyo ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Bw. Selehe Juma, ameipongeza kamati hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya na kusisitiza umuhimu wa kui...

DKT. BASHIRU AGEUKA ‘MBOGO’ NARCO KUKOSA DAWA ZA MIFUGO

Picha
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa ameitaka Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kushirikiana na Idara ya Huduma ya Mifugo na Wakala ya Maabara ya Veterinari Tanzania (TVLA) kwa ajili ya kuangalia upatikanaji wa dawa za mifugo kuhudumia ranchi hiyo  iliyopo Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma na wafugaji wengine kwa ujumla kuzunguka eneo hilo. Agizo hilo amelitoa leo Februari 26, 2026 wakati akizungumza na kusikiliza changamoto za wafugaji na wawekezaji wadogo waliopewa vitalu ndani ya NARCO Kongwa ambapo Dkt. Bashiru amemwagiza pia Katibu Mkuu wa Wizara yake, kusimamia umoja kwa watendaji pamoja na taasisi zake ili kuiendeleza sekta ya mifugo na uvuvi. “Wizara hii ni moja na Waziri wake ni mmoja na aliyemteua Waziri wenu ni Rais huyo mmoja halafu tunashindwa kufanya kazi kama timu moja kwanini?. Watu wa chanjo wako kwenye ofisi yangu, chanjo zinatoka ofisini kwangu, Mkuu wa Madakatari wote wa mifugo yuko kwangu, anayedhibiti dawa za mifugo nchi nzima yuko ofi...

SERIKALI KUSHIRIKIANA NA CHUO CHA MINNESOTA KUWAJENGEA UWEZO WATAALAM WA MIFUGO

Picha
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Minnesota cha Nchini Marekani, imeendelea kujadiliana na kuimarisha mahusiano yenye lengo la kuwajengea uwezo wataalam wa sekta ya mifugo kupitia mradi wa CAHFS ProgRESSVet ili kuhakikisha wataalam hao wanatoa huduma za afya ya wanyama zinazokidhi viwango vya kimataifa. Hatua hiyo inafuatia ujio wa wataalam kutoka Kituo cha Afya ya Wanyama na Usalama wa Chakula cha Minnesota kwa ajili ya kujadili mashirikiano mapya ya mafunzo katika eneo la usalama wa chakula, Majadiliano yaliyo fanyika leo, Februari 25, 2026, katika Makao Makuu ya Wizara yaliyopo Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma. Ujumbe huo uliongozwa na Naibu Mkurugenzi wa CAHFS, Dkt. Maria Perez, na kupokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena, ambaye alisisitiza dhamira ya serikali katika kuendeleza ushirikiano huo. “Serikali itaendelea kushirikiana na Chuo Kikuu cha Minnesota kuhakikisha wataalam wetu wa mifugo wanapata mafunzo ...

VCT YAWATAKA WATOA HUDUMA ZA AFYA YA WANYAMA KUJISAJILI

Picha
Baraza la Veterinari Tanzania (VCT) limewataka wamiliki wa Vituo vya kutoa Huduma za Wanyama pamoja na Wataalam wake kujisajili katika Baraza ili waweze kutambulika na Baraza hilo. Akizungumza kwa niaba ya Msajili wa Baraza la Veterinari Tanzania (VCT), wakati wa Ukaguzi wa Vituo mbalimbali vya kutolea Huduma za Afya ya Wanyama pamoja na Wataalam wake, leo Februari 24, 2026 Mkoani Dar es Salaam, Mkaguzi wa Baraza hilo, Dkt. George Mtinda, amesema takwa la kusajili Wataalam na Vituo vya Huduma za Afya ya Wanyama ni takwa la kisheria ambalo linamtaka Mtaalam au mtoa Huduma hizo kujisajili ili kutambulika na Baraza. "hii ni moja ya utekelezaji wa Sheria ya Veterinari SURA 319, ambayo inawataka Wataalam na Vituo vya kutolea Huduma hizo kujisajili ili kujua kama wamekidhi vigezo katika kutoa huduma.” amesema Dkt. Mtinda Aidha, Dkt. Mtinda amebainisha kuwa ni vyema kuhakikisha watoa Huduma wote wa Afya za Wanyama wanasajili Vituo vyao pamoja na kutumia Wataalam wenye sifa na waliojasili...

GHARAMA ZA UZALISHAJI NA USAFIRISHAJI MAZAO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KUPUNGUA

Picha
Serikali imelenga kupunguza gharama za uzalishaji na usafirishaji wa mazao katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi ili kuongeza thamani na kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi ili kuongeza kipato cha wakulima, wafugaji na wavuvi. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano Uendelezaji na ukuzaji wa shoroba za Kilimo, Mifugo, na Uvuvi uliofanyika February 20, 2026, mkoani Mtwara, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Rajab amesema mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ina fursa kubwa za kimkakati katika utekelezaji wa shoroba za kilimo, Mifugo na Uvuvi kutokana na rasilimali Ardhi na Bahari pamoja na maziwa katika mikoa hiyo. “Mikoa hii ina fursa kubwa za kimkakati katika utekelezaji wa Shoroba za kilimo kutokana na rasilimali zilizopo, mazao ya kipaumbele ambayo ni korosho, ufuta, mbaazi pamoja na  choroko yanayozalishwa zaidi katika Mikoa ya Lindi na Mtwara vilevile mazao ya mahindi, maharage, kahawa, soya na tumbaku yanazalishwa zaidi katika Mkoa wa Ruvuma” amesema Mhe. Rajab. Aidha Mhe. Raja...

MRADI WA MALISHO J-CRISD WAANZA KUTEKELEZWA CHAMWINO

Picha
Mradi wa Uoteshaji wa Malisho ya Mifugo aina ya Juncao na Ustahimilivu wa Tabianchi (J-CRISD) unaofadhiliwa na IDN Norway umeanza kutekelezwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na IDN Africa pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, ambapo wafugaji wanapatiwa mafunzo ya kulima malisho kwa njia ya mashamba darasa. Uzinduzi wa utekelezaji wa mradi huo umefanyika Februari 19, 2026 katika shamba la mfugaji Mayunga Mashishanga lililopo Kata ya Mpayungwa, Katika uzinduzi huo, Afisa Usimamizi wa Nyanda za Malisho Bw. Boniphace Shija, alimwakilisha Mkurugenzi wa Malisho na Rasilimali za Vyakula vya Mifugo na kutoa wito kwa wafugaji kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa mradi huo. “Zao hili tunalolipanda linalenga kusaidia upatikanaji wa malisho ya kutosha, pamoja na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, nitumie fursa hii kulishukuru Shirika la IDN Africa kwa kuwezesha utekelezaji wa shughuli hii, hivyo wafugaji mtoe ushirikiano,” alisema Bw. Shija. Aidha, Meneja...

“UWAZIRI” WANGU HAUNA MAANA KAMA HAUBADILI MAISHA YA WAFUGAJI-DKT. BASHIRU

Picha
◼️Aagiza Tanga Fresh ifanyiwe ukaguzi wa kiuchunguzi  Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amesema kuwa kiapo alichokula wakati akiteuliwa kushika wadhifa huo kinamtaka kusimamia maslahi ya wafugaji ikiwa ni pamoja na kuwaondoa kwenye ufukara na kudhibiti matapeli wanaodhulumu wafugaji. Balozi Dkt. Bashiru amesema hayo wakati wa kikao chake kilicholenga kutathmini hali ya utendaji na kutafuta suluhu ya kukinusuru kiwanda cha kusindika maziwa cha Tanga Fresh kilichofanyika Februari 18,2026 jijini Tanga. “Uwaziri wangu hauna maana kama maziwa ya wafugaji yanamwagwa, Uwaziri wangu hauna maana kama wafugaji ni mafukara, Uwaziri wangu hauna maana kama matapeli wanadhulumu wafugaji” Amesema Balozi Dkt. Bashiru. Balozi Dkt. Bashiru amebainisha kuwa kiapo chake kinamlazimisha kusimamia sekta ya Mifugo ili iendeshwe kwa tija, kibiashara, kwa ufanisi na kwa maslahi ya wafugaji na Taifa. Akielezea maazimio yaliyotokana na kikao hicho, Balozi Dkt. Bashiru pamoja na m...

TASFAM YATAJWA KUAKISI DIRA YA TAIFA

Picha
Na. Edward Kondela Imeelezwa kuwa Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), lazima uakisi matarajio ya dira ya maendeleo ya taifa katika kukuza sekta ya uvuvi nchini. Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Mohammed Sheikh, amebainisha hayo leo (19.02.2026) jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao kazi cha watumishi wanaohudumu katika mradi huo na watendaji wakuu wa taasisi za sekta ya uvuvi, ambapo amesisitiza mradi huo lazima utoe matokeo makubwa kwa wadau wa sekta ya uvuvi hususan vijana na wanawake. Prof. Sheikh ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo katika sekta ya uvuvi, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa maelekezo kadhaa kuhusu sekta ya uvuvi katika matukio mbalimbali hivyo lazima maelekezo yake yatekelezwe kufikia malengo ya kukuza sekta hiyo. Ameongeza kuwa mradi wa TASFAM ni mkubwa katika sekta ya uvuvi, ambao unaweza kubadilisha maisha ya watanzania hususan wavuvi wadogo w...