MAENDELEO YA UJENZI WA SOKO LA SAMAKI KIPUMBWI HAYARIDHISHI - PROF. SHEIKH
Na. Stanley Brayton
◾Wizara yagoma kuzungumzia kuongeza Mkataba.
◾Awashauri wataalam wa Halmashauri kufuatililia kwa karibu Maendeleo ya Mradi.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Prof. Mohammed Ali Sheikh amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya World Class Engineering Contractors Limited kumaliza Ujenzi wa Mradi wa soko la Samaki Kipumbwi haraka iwezekanavyo ili kuweza kuwapa nafasi wavuvi wanaotegemea Soko ilo katika kukuza vipato vyao kwa kufanya biashara, Mradi ambao unatekelezwa chini ya Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kilimo (IFAD).
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, katika ziara yake ya kikazi Mkoani Tanga na kukagua Maendeleo ya Miradi wa Soko la Samaki la Kipumbwi lililopo Wilayani Pangani, leo Februari 27, 2026, Prof. Sheikh amesema soko la Samaki la Kipumbwi ni tegemo kubwa sana kwa wavuvi na ni soko ambalo litasaidia kukuza Uchumi wa wananchi na wa Taifa kiujumla.
"ni vyema Mkandarasi kuhakikisha kasi ya Ujenzi inaongezeka kutoka asilimia 28% kwenda asilimia 80% ndani ya wiki mbili, na hii itawezekana kwa kuongeza kasi ya uletaji vifaa vya Ujenzi eneo la Ujenzi ili kuweza kumaliza Ujenzi wa soko hili kwa wakati.” amesema Prof. Sheikh
Aidha, Prof. Sheikh amemtaka Mkandarasi kuongeza nguvu kazi katika eneo la ujenzi na kufanya kazi usiku na mchana ili kumaliza na kuweza kufikia malengo ya Mradi kwa wakati, maana Wizara haitakuwa na maongezi nao ya kuzungumzia kuhusu kuongeza Mkataba wao.
Vilevile, Prof. Sheikh amemtaka mkandarasi kufika Ofisi za Wizara haraka na mapema hili kuweza kujadiliana ni namna gani wataweza maliza Ujenzi kwa haraka zaidi, na kuleta hati za malipo haraka ili waweze kulipwa mapema.
Pia, Prof. Sheikh ameitaka Idara ya Maendeleo ya Miundombinu ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuimarisha Usimamizi wa Mradi huo kwa kuweka Mhandisi toka Wizarani atakesimami Mradi huo, pamoja na kuhakikisha wakandarasi wanakuwepo eneo la Mradi, kwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka Masoko ya Mazao ya Uvuvi yaongezeke ili kuleta tija kwa Taifa na wavuvi pia.
Prof. Sheikh amewashauri wataalam wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani kufuatililia kwa ukaribu Maendeleo ya Mradi huo ili kuweza kufanikisha Mradi kwa haraka zaidi.



Maoni
Chapisha Maoni