SERIKALI KUSHIRIKIANA NA CHUO CHA MINNESOTA KUWAJENGEA UWEZO WATAALAM WA MIFUGO

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Minnesota cha Nchini Marekani, imeendelea kujadiliana na kuimarisha mahusiano yenye lengo la kuwajengea uwezo wataalam wa sekta ya mifugo kupitia mradi wa CAHFS ProgRESSVet ili kuhakikisha wataalam hao wanatoa huduma za afya ya wanyama zinazokidhi viwango vya kimataifa.

Hatua hiyo inafuatia ujio wa wataalam kutoka Kituo cha Afya ya Wanyama na Usalama wa Chakula cha Minnesota kwa ajili ya kujadili mashirikiano mapya ya mafunzo katika eneo la usalama wa chakula, Majadiliano yaliyo fanyika leo, Februari 25, 2026, katika Makao Makuu ya Wizara yaliyopo Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.

Ujumbe huo uliongozwa na Naibu Mkurugenzi wa CAHFS, Dkt. Maria Perez, na kupokelewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agnes Meena, ambaye alisisitiza dhamira ya serikali katika kuendeleza ushirikiano huo.

“Serikali itaendelea kushirikiana na Chuo Kikuu cha Minnesota kuhakikisha wataalam wetu wa mifugo wanapata mafunzo stahiki yatakayowawezesha kutoa huduma bora na zinazokidhi viwango vya kimataifa,”amesema Bi. Meena.

Kwa upande wake, Dkt. Perez amepongeza ushirikiano uliopo na kubainisha umuhimu wa programu hiyo katika kuimarisha sekta ya mifugo nchini Tanzania.

“Kupitia ProgRESSVet, tunalenga kujenga uwezo wa wataalam wa mifugo ili kuimarisha afya ya wanyama, usalama wa chakula na uchumi wa mifugo kwa ujumla,” amesema Dkt. Perez.

Hadi sasa, jumla ya wataalam 15 wa mifugo wamepata mafunzo katika awamu ya kwanza ya programu hiyo, huku awamu ya pili ikitarajiwa kuwahusisha wataalam 25 zaidi wanaotoa huduma za afya ya wanyama nchini.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena (watatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Ujumbe wa Chuo Kikuu cha Minnesota cha Marekani baada ya Majadiliano yaliyofanyika Ofisini Kwake, Mtumba Dodoma Leo 25 Februari 2026.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena akizungumza na Ujumbe wa Chuo Kikuu cha Minnesota kuhusu ushirikiano baina ya wizara na chuo hicho, katika kutoa mafunzo kwa wataalam wa mifugo, majadiliano hayo yamefanyika Ofisini Kwake Mtumba Jijini Dodoma 25 Februari 2026.

Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo Dkt. Benezeth Lutege akielezea hali ya huduma za mifugo inavyoendelea nchini wakati wa Ujumbe wa Chuo Kikuu cha Minnesota cha Marekani ulipofika kujitambulisha kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Makao Makuu ya Wizara, Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma 25 Februari 2026.

Naibu Mkurugenzi wa Kituo cha Afya ya Wanyama na Usalama wa Chakula (CAHFS) cha Chuo Kikuu cha Minnesota Dkt. Maria Perez akielezea kuhusu mradi wa mafunzo kwa wataalam wa Mifugo wakati wa majadiliano na Katibu Mkuu Bi. Agnes Meena yaliyofanyika wizarani, Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma 25 Februari 2026.

Mtafiti kutoka Kituo cha Afya ya Wanyama na Usalama wa Chakula (CAHFS) cha Chuo Kikuu cha Minnesota Bi. Mary Katherine akieleza jinsi chuo hicho kinavyotoa mafunzo kwa wataalam wa mifugo wakati majadiliano na Katibu Mkuu Bi. Agnes Meena  yaliyofanyika leo 25 Februari 2026

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena (Katikati) akizungumza na Ujumbe wa Chuo Kikuu cha Minnesota kuhusu ushirikiano baina ya wizara na chuo hicho, katika kutoa mafunzo kwa wataalam wa mifugo, majadiliano hayo yamefanyika Ofisini Kwake Mtumba Jijini Dodoma 25 Februari 2026.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO