GHARAMA ZA UZALISHAJI NA USAFIRISHAJI MAZAO YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KUPUNGUA

Serikali imelenga kupunguza gharama za uzalishaji na usafirishaji wa mazao katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi ili kuongeza thamani na kuvutia uwekezaji wa sekta binafsi ili kuongeza kipato cha wakulima, wafugaji na wavuvi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano Uendelezaji na ukuzaji wa shoroba za Kilimo, Mifugo, na Uvuvi uliofanyika February 20, 2026, mkoani Mtwara, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Rajab amesema mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma ina fursa kubwa za kimkakati katika utekelezaji wa shoroba za kilimo, Mifugo na Uvuvi kutokana na rasilimali Ardhi na Bahari pamoja na maziwa katika mikoa hiyo.

“Mikoa hii ina fursa kubwa za kimkakati katika utekelezaji wa Shoroba za kilimo kutokana na rasilimali zilizopo, mazao ya kipaumbele ambayo ni korosho, ufuta, mbaazi pamoja na  choroko yanayozalishwa zaidi katika Mikoa ya Lindi na Mtwara vilevile mazao ya mahindi, maharage, kahawa, soya na tumbaku yanazalishwa zaidi katika Mkoa wa Ruvuma” amesema Mhe. Rajab.

Aidha Mhe. Rajab ameongeza kuwa Serikali kupitia Wizara za Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mageuzi ya Kilimo (ATO) na (AGCOT) inaendelea kuratibu utekelezaji wa miradi ya kimkakati nchini kwa kuzingatia matumizi ya tekinolojia za kisasa, huduma za Ugani, pembejeo za kilimo, ushiriki wa vijana na wanawake pamoja na kuzingatia manadiliko ya tabia ya nchi.

Pia amesema kuwa utekelezaji wa mpango huo ni nyenzo ya kimkakati katika utekelezaji wa Agriculture Master Plan (AMP 2050) mpango huo umebuniwa ili kuunganisha maeneo yenye uzalishaji mkubwa na miundombinu muhumu ya barabara, reli, bandari, masoko, na viwanda pamoja na huduma za kifedha. 

Mhe. Zainab Rajab amesisitiza kuwa mkutano huo utawawezesha  wataalam kuelewa kwa kina dhana ya Shoroba za kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na wajibu wao katika utekelezaji wake na namna ya kuzitafsiri Sera na Mipango ya Kitaifa kuwa ni miradi yenye matokeo chanya kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Rajab akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa mkutano wa uhamasishaji wa ukuzaji na uendelezaji wa shoroba za Kilimo, Mifugo na Uvuvi uliofanyika February 20, 2026, mkoani Mtwara.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Abdallah Mwaipaya akichangia jambo wakati wa mkutano wa uhamasishaji wa ukuzaji na uendelezaji wa shoroba za kilimo, mifugo na uvuvi uliofanyika February 20, 2026, mkoani Mtwara.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuendeleza Shoroba za Kilimo Tanzania (AGCOT) Bw. Geofrey Kirenga akizungumza jambo wakati wa mkutano wa uhamasishaji wa ukuzaji na uendelezaji wa shoroba za Kilimo, Mifugo na Uvuvi uliofanyika February 20, 2026, mkoani Mtwara.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO