BI. MEENA AONGOZA KIKAO CHA MAGEUZI YA SEKTA YA MAZIWA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agness Meena, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utekelezaji wa Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi, leo Februari 27, 2026, jijini Dar es Salaam ameongoza kikao muhimu cha wajumbe wa kamati hiyo kutoka Tanzania Bara na Visiwani.

Kikao hicho kililenga kupitia kwa pamoja hatua za utekelezaji wa mradi tangu kuanza kwake hadi sasa, pamoja na kujadili mikakati madhubuti ya kuendeleza utekelezaji wake kwa ufanisi zaidi.

Bi Meena amesisitiza kwa wajumbe pamoja na sekretarieti ya kamati umuhimu wa kuwa na mgawanyo sahihi wa majukumu, ushirikiano wa karibu pamoja na mawasiliano yenye tija. Hatua hizi ni muhimu ili kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa wakati na kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Mwenza wa kamati hiyo ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Bw. Selehe Juma, ameipongeza kamati hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania Bara na Visiwani katika kutekeleza mradi huo.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi. Agness Meena, akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Mifugo), Dkt. Fabian Magawa, wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi wa Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi, kilichofanyika tarehe 27 Februari 2026 jijini Dar es Salaam

Baadhi ya wajumbe pamoja na Sekretarieti ya Mradi wa Mageuzi ya Tasnia ya Maziwa na Mabadiliko ya Tabianchi wakiwa kwenye kikao cha mapitio na majadiliano ya utekelezaji wa mradi huo, kilichofanyika tarehe 27 Februari 2026 jijini Dar es Salaam.




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO