TASFAM YATAJWA KUAKISI DIRA YA TAIFA

Na. Edward Kondela

Imeelezwa kuwa Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), lazima uakisi matarajio ya dira ya maendeleo ya taifa katika kukuza sekta ya uvuvi nchini.

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Mohammed Sheikh, amebainisha hayo leo (19.02.2026) jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao kazi cha watumishi wanaohudumu katika mradi huo na watendaji wakuu wa taasisi za sekta ya uvuvi, ambapo amesisitiza mradi huo lazima utoe matokeo makubwa kwa wadau wa sekta ya uvuvi hususan vijana na wanawake.

Prof. Sheikh ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo katika sekta ya uvuvi, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa maelekezo kadhaa kuhusu sekta ya uvuvi katika matukio mbalimbali hivyo lazima maelekezo yake yatekelezwe kufikia malengo ya kukuza sekta hiyo.

Ameongeza kuwa mradi wa TASFAM ni mkubwa katika sekta ya uvuvi, ambao unaweza kubadilisha maisha ya watanzania hususan wavuvi wadogo wadogo na kuwataka watumishi wanaohudumu katika mradi huo kutumia muda mwingi kufanya matayarisho pamoja na kuwa na mipango inayotekelezeka.

Aidha, ametaka matumizi ya weledi, rasilimali na muda stahiki ili kufikia matarajio ya viongozi wa juu katika kuchangia sekta ya uvuvi kupitia uchumi wa buluu na sekta ya uvuvi kwa ujumla.

Nao baadhi ya wajumbe kwenye kikao kazi hicho wamepata fursa ya kutoa maoni yao namna idara na taasisi za wizara katika sekta ya uvuvi, zitakavyoshiriki vyema katika mradi huo ili kupatikana matokeo chanya kwa taifa. 

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Mohammed Sheikh akifafanua namna Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM), utakavyoakisi matarajio ya dira ya maendeleo ya taifa katika kukuza sekta ya uvuvi nchini, wakati wa kikao kazi cha watumishi wanaohudumu katika mradi huo na watendaji wakuu wa taasisi za sekta ya uvuvi, jijini Dar es Salaam. (19.02.2026)

Mratibu wa Mradi wa Utekelezaji wa Rasilimali za Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji (TASFAM) Tanzania Bara, Dkt. Nichrous Mlalila, akifafanua baadhi ya mambo juu ya utekelezaji wa mradi huo wakati wa kikao kazi cha watumishi wanaohudumu katika mradi huo na watendaji wakuu wa taasisi za sekta ya uvuvi, jijini Dar es Salaam. (19.02.2026)




Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

LESENI, VIBALI VYA MAZAO YA MIFUGO NA VYAKULA VYA SAMAKI KUTOLEWA KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

DKT. MHEDE AONGOZA ZOEZI LA UCHANJAJI WA MIFUGO MKOANI IRINGA, WAFUGAJI WAPONGEZA HATUA YA SERIKALI

SERIKALI KURASIMISHA BIASHARA YA MABONDO