Jumapili, 30 Aprili 2023
Jumamosi, 29 Aprili 2023
MTAMBO WA KUZALISHA KIMIMINIKA NAIC WAZINDULIWA.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe, amemshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuridhia jumla ya fedha Milioni 300 kwa ajili ya kununua mtambo wa Kimiminika (Liquid Nitrogen) kwa ajili ya kuhifadhia mbegu bora za ng'ombe.
Prof.Shemdoe ameyasema hayo Jana 28 April, 2023 wakati akizindua Mtambo huo wa Kuzalisha Kikiminika (Liquid Nitrogen) kwa ajili ya kutunzia mbegu bora za ng'ombe wa nyama na maziwa katika kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC) Arusha.
"Tunamshukuru sana Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuridhia jumla ya fedha Milioni 300 ili kujazia katika fedha iliyotolewa na Bill & Melinda Gates Foundation Tsh milioni 432 kupitia shirika lisilokuwa la kiserikali la Land O'lakes na kufanya jumla ya Tsh 732 milioni zitumike kununua mtambo huo."Alisema Prof. Shemdoe.
Prof. Shemdoe amesema kuwa kuwepo kwa mtambo huo sasa katika kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC) utasaidia kuleta tija hasa katika kuzalisha ng'ombe bora wa Nyama na Maziwa hapa Tanzania.
"Kwa uwepo wa Mtambo huu hapa NAIC sasa utasaidia kuboresha Mifugo yetu, hivyo kuongeza Uwingi wa nyama bora na maziwa kwani tayari soko la nyama lipo, kwahiyo tukiboresha Mifugo yetu tutapata nyama nyingi na yenye viwango hivyo tutauza nje ya nchi na kuongeza mchango wa Sekta ya Mifugo katika Pato la Taifa." Alisema Prof. Shemdoe.
Aidha, Shemdoe amesema kuwa zaidi ya asilimia 95 ya ng'ombe waliopo hapa nchini ni wa asili wenye uzalishaji Mdogo, kwahiyo amesema kuwa zinahitajika juhudi za Makusudi kuongeza kundi la ng'ombe wanaozalisha nyama na Maziwa kwa wingi ili kutoshereza mahitaji yanayoongezeka ya walaji wa Nyama na Maziwa.
"Azma ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuboreha Mbari za Mifugo, Serikali imenunua Madume matatu (3) ya kisasa kutoka Afrika ya kusini pamoja na kuhakikisha kituo hiki cha NAIC kinakuwa kituo bora cha kuzalisha mbegu za Mifugo Afrika Mashariki na ikiwezeka mbegu hizi ziuzwe hata nje ya nchi."Alisema Prof. Shemdoe.
Awali Kaimu Mkurugenzi wa kituo Cha Taifa Cha uhimilishaji (NAIC) Dkt. Dafay Bura, alimweleza Prof. Shemdoe kuwa kwa sasa kituo kina jumla ya madume bora 34 ambayo yameganyika katika sehemu nne ambazo ni, Madume ya mbegu ya ng'ombe wa Maziwa, Nyama na Maziwa (Dual Purpuse), Nyama (Beef) na Cross breed.
Halikadharika, Bill & Melinda Gates pamoja na Land O'lakes wamesema kuwa wamefurahishwa kuona mtambo huo wa kuzalisha kimiminika (Liquid Nitrogen) unafanya kazi Vizuri bila shida yoyote, hivyo wanamatumaini makubwa ya kuona wafugaji wanahimilisha mifugo yao ili kujiletea tija mfugaji mmoja mmoja na hatimaye kuchangia katika pato la Taifa.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Riziki Shemdoe (kushoto) akishuhudia Kimiminika (Liquid Nitrogen) akizalishwa.Wengine katika picha ni Watumishi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe (kulia) akikata Utepe Jana 28 April 2023 kuashiria uzinduzi wa mtambo wa kuzalisha kimiminika (Liquid Nitrogen) katika kituo cha taifa cha Uhimishaji (NAIC) Arusha.Wengine katika picha kutoka kushoto ni Dkt.Afred De Vries, Program officer BMGF, Dai Harvey, Group Director kutoka Land O'Lakes.
Mtambo wa kuzalisha kimiminika (Liquid Nitrogen) uliozinduliwa jana tarehe 28 April 2023 na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe.
KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA TAASISI YA UTAFITI WA MIFUGO TANZANIA (TALIRI) CHAFANYIKA JIJINI DODOMA
Naibu Katibu Mkuu (Uvuvi) Bi. Agness Meena akisoma hotuba kwa Niaba ya Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe wakati wa ufunguzi wa kikao cha baraza la wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kilichofanyika kwenye ukumbi wa African dream jijini Dodoma Aprili 28, 2023.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa MifugoTanzania (TALIRI), Prof. Erick Komba akiongea na wajumbe wa baraza la wafanyakazi TALIRI wakati wa kikao kifupi kilichofanyika jijini Dodoma Aprili 28,2023.
Katibu wa Chama cha wafanyakazi wa Taasisi za elimu ya juu, Sayansi, Ufundi stadi, habari na Utafiti (RAAWU), Bw. Bakari Shekimweri akieleza lengo la kuwa na chama cha wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kudumisha ushirikiano miongoni mwao wakati wa kikao kifupi cha wajumbe wa wafanyakazi hao kilichofanyika kwenye ukumbi wa African dream jijini Dodoma Aprili 28,2023.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Utafiti, mafunzo na Ugani sehemu ya Huduma za Ugani, Bw. Samwel Mdachi akitoa neno kwa wajumbe wa baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) (hawapo pichani) wakati wa kikao kifupi kilichofanyika jijini Dodoma, Aprili 28,2023.
Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Bi. Agness Meena (wa tano kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) mara baada ya kikao kifupi kilichofanyika kwenye ukumbi wa African dream jijini Dodoma Aprili 28,2023.
NDOTO YA RAIS, DKT. SAMIA KUIFUFUA NARCO YAANZA KUTIMIA
Na Mbaraka Kambona,
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeiwezesha Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO) kiasi cha Shilingi bilioni 4.65 kwa ajili ya kununua vitendea kazi na ng'ombe wazazi ili kuboresha na kuongeza uzalishaji wa kampuni hiyo.
Hayo yamefahamika wakati wa ziara ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega aliyoifanya katika Ranchi ya Kongwa iliyopo Wilayani Kongwa, jijini Dodoma Aprili 27, 2023.
Wakati akizindua matreka mapya matano (5) na kupokea ngo'mbe elfu moja (1000) kwa ajili ya kuboresha uzalishaji wa kampuni ya NARCO, Mhe. Ulega alimshukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha kampuni hiyo ili iweze kujiendesha kibiashara.
Alisema lengo la Rais, Dkt. Samia ni kuiimarisha NARCO kwa kuboresha miundombinu na vitendea kazi ili waweze kunenepesha ng'ombe, kuimarisha biashara ya nyama bora ya Kongwa Beef na kuzalisha malisho ya mifugo kwa wingi na kuyauza ndani na nje ya nchi.
"Hivi sasa tumeshafika katika kiwango cha kuuza nje ya nchi nyama Tani Elfu 12, na kuanzia mwaka ujao na kuendelea tutatoka kwenye Tani Elfu 12 na kutafuta Tani Elfu 50 na ikiwezekana mpaka Tani Laki moja", alisema
Aliendelea kusema kuwa katika mkakati wa kuifufua kampuni ya NARCO pia wataanzisha skimu za unenepeshaji wa mifugo ili nyama itakayokuwa inazalishwa kutoka NARCO iwe na ubora wa kuiuza nje ya nchi.
"Tunakusudia kwamba mchango wa sekta ya mifugo uongezeke kutoka asilimia 7 Hadi kufikia asilimia zaidi ya 10, na hilo linawezekana kwa sababu rasilimali ya kutuwezesha kufikia huko tunayo", alisisitiza
Aidha, alisema kuwa Serikali ina mipango ya kuanzisha skimu za umwagiliaji wa malisho ili yaweze kuzalisha kwa wingi kwa ajili ya kuyauza ndani na nje ya nchi.
"Kama ambavyo huwa tunasafirisha mahindi kutoka maeneo mbalimbali na kuwapelekea wahitaji tunataka pia tuzalishe malisho kwa wingi na kuyasafirisha kuyapeleka kwa wahitaji waliopo ndani na nje ya nchi", alifafanua
Mkurugenzi Mkuu, Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Prof. Peter Msoffe (kushoto) akimuonesha Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega (katikati) sehemu ya vifaa walivyovinunua kwa ajili ya kuzalisha malisho ya mifugo wakati Waziri huyo alipofanya ziara katika Ranchi ya Kongwa iliyopo Wilayani Kongwa, jijini Dodoma Aprili 27, 2023. (Kulia) ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Daniel Mushi.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akimueleza jambo Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Remidius Emmanuel (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake Wilayani Kongwa, jijini Dodoma Aprili 27, 2023. (Kulia) ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Daniel Mushi.
Ijumaa, 28 Aprili 2023
KIKAO KIFUPI CHA KUPOKEA WASILISHO LA MKAKATI WA UFUATILIAJI WA KIELEKTRONIKI WA ZAO LA PWEZA CHAFANYIKA WILAYANI YA KILWA, MKOA WA LINDI
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora na Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bw. Melkizedeck Koddy akiongea na watendaji kutoka Sekta ya Uvuvi na wawakilishi kutoka kwenye mradi wa Aqua - Farms wakati wa kikao kifupi cha kupokea wasilisho la mkakati wa ufuatiliaji wa kielektroniki wa zao la Pweza katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma. Aprili 25, 2023
Mtafiti kutoka kwenye Mradi wa Aqua-farm , Bw. Cretus Philipo akiwasilisha mkakati wa ufuatiliaji wa kielektroniki wa zao la Pweza, uliofanyika Wilayani Kilwa Mkoani Lindi, wakati wa kikao kifupi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mtumba jijini Dodoma, Aprili 25,2023.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia kwa makini wasilisho la mkakati wa ufuatiliaji wa kielektroniki wa zao la Pweza lililofanyika kwenye Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi wakati wa kikao kifupi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mtumba jijini Dodoma, Aprili 25, 2023
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Udhibiti Ubora na Masoko Bw. Melkizedeck Koddy (wa pili kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji kutoka Sekta ya Uvuvi na wawakilishi kutoka kwenye mradi wa Aqua-farm, mara baada ya kikao kifupi cha kuwasilisha mkakati wa ufuatiliaji wa kielektroniki wa zao la Pweza katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Wizara hiyo mtumba jijini Dodoma, April 25,2023.
MIL 1O KWA KILA KIJANA KUFUGA KIBIASHARA
Na. Edward Kondela
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda amewaasa watanzania hususan vijana wanaopatiwa mafunzo ya unenepeshaji mifugo na Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo baada ya mafunzo hayo ya mwaka mmoja kila mmoja ataondoka na mtaji usiopungua Shilingi Milioni Kumi kufanya ufugaji kibiashara.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Pinda ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Baraza la Kumshauri Rais Kuhusu Utekelezaji wa Masuala ya Kilimo na Chakula amebainisha hayo (24.04.2023), wakati alipofanya ziara ya siku moja Mkoani Tanga, kutembelea vituo atamizi vya wizara hiyo vinavyotekelezwa kupitia Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) kwa ajili ya kutoa mafunzo ya vitendo ndani ya mwaka mmoja kwa vijana juu ya unenepeshaji ng’ombe katika kipindi cha miezi mitatu.
Akiwa katika vituo hivyo kwa nyakati tofauti amesema ni vyema baada ya mafunzo vijana hao waliopo kwenye vituo atamizi vinane (8) kwenye maeneo mbalimbali nchini kufahamika katika mikoa wanayotoka ili wakitafutwa watoe taarifa wametoa faida gani kwa wafugaji wengine, ambao watakuwa wamebadilika kibiashara.
Ameongeza kuwa ufugaji wa kibiashara ni muhimu kwa vijana hao kuzingatiwa kwa kutoa elimu waliyopata kwa wafugaji ya namna bora ya kuchagua mifugo minadani na kuipatia malisho bora vikiwemo vyakula vya ziada ili kuwanenepesha na kuuza kwa faida baada ya miezi mitatu.
“Kumbe kilimo hiki au ufugaji huu ni biashara kwa uhakika, ng’ombe uliyemnunua Laki Mbili (2) unakuja kumnenepesha kwa miezi mitatu baadaye unakuja kumuuza Milioni Mbili kwa nini usihangaike nalo hili?, Mwaka mzima unaniachia Milioni Kumi kwa nini nisifanye?” amesema Mhe. Pinda
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde amesema kuanzishwa kwa programu ya vituo atamizi ni maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan lengo likiwa ni kuboresha Sekta ya Mifugo kuwa ya kisasa na kuleta tija zaidi.
Ameongeza kuwa kijana atayakayemaliza pogramu ya unenepeshaji mifugo hususan ng’ombe itakayodumu kwa mwaka mmoja atapatiwa na serikali Shilingi Milioni Kumi za mtaji na kwamba fedha hizo siyo mkopo bali aende kujiendeleza katika ufugaji kibiashara.
Ametoa rai kwa watanzania kumuunga mkono Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa anajihusisha na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja ili kuboresha maisha ya wananchi.
Naye Mwakilishi wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo Dkt. Angello Mwilawa ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani amemwambia Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda namna wizara ya Mifugo na Uvuvi inavyoshirikiana na taasisi nyingine za serikali ili vijana kupata mafunzo hayo kupitia mikopo pamoja na uwekaji wa miundombinu pamoja na rasilimali chakula cha mifugo kwa gharama za chini huku mmoja wa vijana wanaopatiwa mafunzo ya unenepeshaji ng’ombe Bi. Happy Samson akisema mtaji atakaopata baada ya kumaliza mafunzo utamwezesha kuanza biashara ya mifugo kwa ufasaha kwa kufuata elimu ya vitendo aliyoipata.
Serikali tayari imetenga Shilingi Bilioni 4.4 katika programu ya vituo atamizi kwenye vituo vinane (8) kote nchini kupitia Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) na Taasisi ya Utafiti wa Mifyugo Tanzania (TALIRI), ambapo hadi Mwezi Machi mwaka huu ng’ombe 865 kati ya 900 wamenunuliwa kwa ajili ya programu hiyo ambayo mpango wa mafunzo ni mwaka mmoja na kila kijana atapata fursa ya kunenepesha mifugo hususan ng’ombe katika mizunguko minne ya ng’ombe kumi (10) kwa kila mzunguko na faida itakayopatikana baada ya kuuza ng’ombe hao itatumika kama mtaji kwa ajili ya kijana mnufaika kwenda kuanzisha miradi kama hiyo.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda (kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde, mara baada ya Waziri Mkuu Mstaafu Pinda kutembelea vituo atamizi katika Mkoa wa Tanga vilivyopo Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tazania (LITA) na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI), ikiwa ni moja ya vituo vinane (8) ambavyo vinatoa mafunzo ya mwaka mmoja kwa vijana namna ya kunenepesha mifugo hususan ng’ombe katika kipindi cha miezi mitatu na kupatiwa na serikali mtaji usiopungua Shilingi Milioni 10 kwa kila mmoja baada ya mafunzo ili kuendeleza mradi huo. (24.04.2023)
Mwakilishi wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo Dkt. Angello Mwilawa ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani amemwambia Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda (hayupo pichani) namna wizara ya Mifugo na Uvuvi inavyoshirikiana na taasisi nyingine za serikali ili vijana kupata mafunzo ya unenepeshaji mifugo hususan ng’ombe katika vituo atamizi kupitia mikopo, uwekaji wa miundombinu pamoja na uwepo wa rasilimali chakula cha mifugo kwa gharama za chini. (24.04.2023)
Muonekano wa baadhi ya ng’ombe 865 kati ya 900 walionunuliwa na serikali kufikia Mwezi Machi mwaka huu kwa ajili ya programu ya vituo atamizi kwa ajili ya vijana kujifunza juu ya unenepeshaji katika vituo vinane (8) nchini kupitia Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) na Taasisi ya Utafiti wa Mifyugo Tanzania (TALIRI), mpango wa mafunzo ni mwaka mmoja na kila kijana atapata fursa ya kunenepesha mifugo hususan ng’ombe katika mizunguko minne ya ng’ombe kumi (10) kwa kila mzunguko na faida itakayopatikana baada ya kuuza ng’ombe hao itatumika kama mtaji kwa ajili ya kijana mnufaika kwenda kuanzisha miradi kama hiyo. (24.04.2023)
Baadhi ya wanafunzi wa unenepeshaji mifugo hususan ng’ombe katika vituo atamizi vya Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) katika Mkoa wa Tanga, wakimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda (hayupo pichani) alipofika katika vituo hivyo kujionea kwa vitendo namna wanafunzi hao wanavyofundishwa juu ya ufugaji bora. (24.04.2023)
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda (katikati), Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Waziri Kindamba na Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde (kulia), wakiwa kwenye mazungumzo juu ya Sekta ya Mifugo, mara baada ya Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Pinda kufanya ziara ya siku moja mkoani humo. (24.04.2023)
Alhamisi, 27 Aprili 2023

JUKUMU LA KUHAKIKISHA UPATIKANAJI WA MALISHO SI LA SERIKALI PEKEE-DKT. MHINA
◼️ SUA yaanza utafiti wa nyasi za asili
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imebainisha kuwa ni wajibu wa kila mdau aliyepo kwenye sekta ya ufugaji kuhakikisha upatikanaji wa malisho na maji ya kutosheleza mahitaji ya mifugo kwa kipindi chote cha mwaka unakuwa ni wa uhakika.
Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Charles Mhina wakati akifungua mkutano wa 13 wa wadau wa Nyanda za malisho nchini (RST) uliofanyika mkoani Morogoro Aprili 24,2023.
“Katika miaka ya karibuni takwimu zimetuonesha kumekuwa na tatizo la ongezeko la vifo vya mifugo vilivyotokana na ukosefu wa malisho na maji katika baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi hivyo kama tusipokabiliana na changamoto hii tutaendelea kupoteza tija kwenye ufugaji wetu” Ameongeza Dkt. Mhina.
Dkt. Mhina ametoa rai kwa Mamlaka za Serikali za mitaa kuendelea kubainisha na kutenga maeneo kwenye halmashauri kwa ajili ya malisho ya mifugo huku pia akiwahimiza wafugaji kununua maeneo yanayokidhi idadi ya mifugo yao, kupanda malisho na kuweka miundombinu ya upatikanaji wa maji ya kutosha.
“Kama kila mfugaji akinunua eneo lake na kulimiliki kwa mujibu wa sheria kisha akapanda malisho ya mifugo yake na kuweka miundombinu ya maji ya kunyweshea mifugo hiyo, tutakuwa tumepiga hatua kubwa kwenye ufugaji wenye tija” Amesema Dkt. Mhina.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha nyanda za malisho nchini (RST) Prof. Selemani Ismail amesema kuwa mkutano huo hulenga kupata maazimio mbalimbali ambayo huwasilishwa kwenye mamlaka mbalimbali ikiwemo Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa ajili ya utekelezaji.
“Nichukue fursa hii kuishukuru Wizara kwani imetekeleza baadhi ya maazimio ya mkutano uliopita ikiwa ni pamoja na lile la uanzishwaji wa mashamba darasa, kutenga maeneo ya malisho, ajira kwa wahitimu wanaomaliza shahada ya usimamizi wa nyanda za malisho na elimu kwa wafugaji wetu ili wafuge ufugaji wenye tija” Amesema Prof. Ismail.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Prof. Raphael Chibunda ameweka wazi zoezi la utafiti wa nyasi za asili linalofanywa na chuo chake mara baada ya kugundua mchango wa malisho hayo kwa wanyamapori kwa mwaka mzima.
“waliotutawala walikuja na kuzipa sifa mbaya nyasi zetu za asili japo ndo hizo hizo zinazotumiwa na wanyama pori kama Tembo, Twiga, Pundamilia na wengineo na wakati wote hata kiangazi huwezi kuwaona wanyama hao wamekonda lakini bahati mbaya sisi tumewekeza nguvu nyingi kidogo sana kwenye nyasi hizo ambazo ndo zinazowatunza wanyama wetu na ndio maana sisi kama chuo tumeamua kuchukua hatua” Amesisitiza Prof. Chibunda.
Mkutano huo wa siku moja hufanyika kila mwaka kwa lengo la kujadili kwa kina tasnia ya uzalishaji wa malisho ya mifugo ili kuhakikisha wafugaji wanafuga kwa tija.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Mhina (kushoto) akimkabidhi cheti mwanafunzi wa Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Bw. Chacha Marwa kwenye mkutano wa Chama cha Nyanda za malisho uliofanyika Aprili 24, 2023, mkoani Morogoro mara baada ya kuibuka mshindi wa uandishi bora wa andiko la biashara kuhusu malisho ya mifugo.
Sehemu ya washiriki wa Mkutano wa wadau wa Nyanda za malisho wakimsikiliza Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Mhina (hayupo pichani) wakati wa Mkutano huo uliofanyika Aprili 24, 2023 mkoani Morogoro.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Mhina (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa wadau wa Nyanda za malisho uliofanyika Aprili 24, 2023 mkoani Morogoro.
SHIRIKIANENI NA MAMLAKA HUSIKA ILI MCHANGO WA SEKTA YA UVUVI UONEKANE – MHE. SILINDE
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde amezisihi nchi wanachama wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuungana na mamlaka zinazoshughulikia viwanda na biashara na takwimu kuhakikisha mchango wa sekta ya uvuvi unaonekana wazi kwenye pato la Taifa la kila nchi.
Mhe. Silinde (Mb.) ametoa wito huo jijini Kampala, Uganda alipozungumza katika Mkutano wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekta ya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Aprili 20,2023 jijini humo.
Mhe. Silinde amesema kuwa suala hilo linatokana na ukweli kwamba mazao yanayotokana na uvuvi yanahesabiwa katika sekta za kilimo na uzalishaji na kuacha mazao mengine yakiingizwa katika mnyororo wa thamani wa sekta nyingine na kusababisha mchango wa sekta ya uvuvi katika uchumi wa nchi uonekane mdogo.
Akizungumzia ulinzi wa rasilimali za uvuvi katika ziwa hilo Mhe. Silinde amesema uvuvi haramu na uvuvi uliopitiliza unahatarisha uwepo endelevu wa rasilimali za uvuvi na mazalia yake katika Ziwa Victoria.
Aidha Mhe. Silinde ameongeza kuwa taarifa zinasema kuwa idadi ya Samaki aina ya Sangara kwa mfano imepungua kwa asilimia 33 katika muda wa mwaka 2021 na 2022 nakuongeza kuwa nchi wanachama wanachama wa LVFO haziwezi kukaa pembeni na kuacha vitendo hivyo vikiendelea kushamiri kwakuwa vinaathiri mamilioni ya watu ambao maisha yao yanategemea ziwa hilo.
Amesema Ziwa Victoria linatoa maji kwa matumizi ya majumbani na kusuapoti shughuli mbalimbali za kiuchumi ukiwemo uvuvi na ukuzaji wa viumbe maji katika nchi zetu na hivyo suala la ulinzi wake ni lazima kutiliwa mkazo.
“Ni wazi kuwa sekta ndogo mbili hizi ni muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi katika nchi zetu zote na mtakubaliana nami kuwa Uvuvi katika Ziwa hilo unatoa ajira, chakula, mapato kwa familia na kuziwezesha familia hizo kuishi pamoja na kuzipatia nchi fedha za kigeni na mapato kwa nchi na hivyo ni lazima kuziangalia kwa umakini,” alisema Mhe. Silinde.
Mhe Naibu Waziri Silinde alitumia Mkutano huo kuipongeza Sekretarieti ya LVFO na nchi wanachama kwa kuunga mkono utekelezaji wa progrmu na miradi ya uvuvi na ukuzaji wa viumbe maji.
Amesema wakati akizipongeza Nchi wanachama na Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) kwa kutekeleza maelekezo na maagizo yaliyotolewa na Mikutano ya Baraza la Mawaziri iliyopita amezitaka kuhakikisha hatua na jitihada za pamoja za kuwalinda Samaki aina ya sangara na rasilimali nyingine zinazopatikana katika ziwa Victoria zinaendelezwa na kuimarishwa.
“Ni wazi kuwa kumekuwa na hatua kubwa katika utekelezaji wa maagizo na maelekzo yanayotolewa na Baraza la Mawaziri, hili linonekana wazi kutokana na idadi ya miradi iliyotekelezwa huu ni ushahidi tosha kuwa sekretarieti ya LVFO iko makini katika kutekeleza maagizo yanayotolewa na Baraza la Mawaziri la sekta, nawapongeza sana,” alisema Mhe. Silinde
Mhe. Silinde pia alipongeza Kamati ya Uratibu inayoongozwa na Makatibu Wakuu kwa kuandaa vyema nyaraka za mkutano wao na hivyo kurahisisha kazi ya Mawaziri katika kikao hicho.
Katika Mkutano huo Tanzania ilikabidhi kijiti cha uenyekiti kwa Uganda na kuipongeza kwa kuchukua nafasi hiyo na hivyo kuitakia utekelezaji mwema wa majukumu yake ya kulinda rasilimali za uvuvi katika Ziwa Victoria.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde akizungumza wakati wa Mkutano wa TANO wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la nchi wanachama wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Kampala Aprili 20 Aprili,2023
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde (wa pili kushoto ) akiwa na Mawaziri kutoka nchi za Uganda, Kenya na Burundi baada ya kumalizika kwa Mkutano wa TANO wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la nchi wanachama wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Kampala Aprili 20, 2023.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. David Silinde (wa pili kutoka kulia) akizungumza na Wajumbe wa Mkutano wa TANO wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la nchi wanachama wa Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Kampala Aprili 20,2023.
TANZANIA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA NCHI ZA EAC KULINDA RASILIMALI ZA UVUVI ZIWA VICTORIA
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhakikisha rasilimali za Ziwa Victoria zinalindwa ili zinufaishe jamii zinazozunguka ziwa hilo na mataifa husika.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na
Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe aliyeongoza ujumbe kutoka Tanzania katika mkutano
huo wa Tano wa Baraza la Mawaziri la Sekya Uvuvi na Ukuzaji Viumbe Maji wa
Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria (LVFO) ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika
ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika tarehe 19 Aprili, 2023 jijini Kampala,
Uganda.
Prof. Shemdoe alisisitiza kuwa Tanzania inaendelea
kudhibiti matumizi ya zana haramu za uvuvi, kupiga marufuku uvuvi wa samaki wachanga,
kudhibiti utoroshaji wa mazao ya uvuvi na kuhamasisha ufugaji wa samaki kwa vizimba
katika Ziwa Victoria bila kuathiri mazingira.
Pia alisema kuwa Tanzania imeimarisha udhibiti wa uingizwaji
wa zana haramu za uvuvi na kuendesha ukaguzi wa kina ili kuhakikisha kunakuwa
na uvuvi endelevu na wenye tija.
Mchango wa Sekta ya Uvuvi katika uchumi wan chi za Jumuiya
ya Africa Mashariki bado ni mdogo kwa kuwa mchango wake haujumuishwi na mapato
yanayotokana na shughuli zote za uvuvi zinazofanyika katika mnyororo wa thamani
badala yake mchango huo unaotokana na mnyororo wa thamani unajumuishwa katika
sekta nyingine.
Mkutano huo umehudhuriwa nan chi wanachama wa Jumuiya ya
Africa Mashariki (EAC) zilizopo katika Taasisi ya Uvuvi ya Ziwa Victoria.
MKURUGENZI MICHAEL AZUNGUMZA NA WATAALAM KUTOKA SUA KUHUSU UWEZEKANO WA KUPATIWA MAENEO KWA AJILI YA KUANZISHA VITUO ATAMIZI
Mkurugenzi, Idara ya Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko, Bw. Stephen Michael (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam kutoka Chuo cha Kilimo (SUA) muda mfupi baada ya kufanya nao majadiliano kuhusu uwezekano wa Wataalam hao kupatiwa sehemu katika maeneo ya kupumzishia mifugo ili waanzishe vituo Atamizi kwa ajili ya kuwafundisha vijana kunenepesha mifugo na kuanzisha Kliniki ya mifugo kwa lengo la kuwasaidia wafugaji.
Kulia kwake ni Kiongozi wa msafara wa Wataalam hao kutoka SUA, Prof. Elliot Phiri. Maeneo ambayo wanapendekeza wapatiwe ni pamoja na eneo la kupumzishia mifugo la Kizota lililopo Dodoma na Makuyuni lililopo Monduli, Mkoani Arusha.
Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi zilizopo katika Jengo la NBC jijini Dodoma Aprili 20, 2023.
Wengine katika picha ni Wataalam kutoka Wizarani na Wataalam wengine kutoka SUA.
DKT. ASIMWE AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI WA MALISHO YA MIFUGO KATIKA SHAMBA LA VIKUGE. AELEZA MIPANGO YA SERIKALI YA KUTATUA CHANGAMOTO YA CHAKULA CHA MIFUGO NCHINI
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho na Rasilimali ya Vyakula vya Wanyama, Dkt. Asimwe Rwiguza (kulia) akikagua maendeleo ya Shamba Darasa la malisho ya mifugo lililopo katika Kijiji cha Wami Sokoine, Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Mkoani Morogoro alipotembelea eneo hilo Aprili 19, 2023. kushoto ni Mjumbe wa kikundi wa shamba darasa hilo, Bw. Jumbe Kamando.
Wizara imeanzisha mashamba darasa 100 katika Halmashauri 44 nchini ili wafugaji waweze kujifunza kwa vitendo namna ya kuandaa, kupanda, kutunza na kuhifadhi malisho ya mifugo.
Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho na Rasilimali ya Vyakula vya Wanyama, Dkt. Asimwe Rwiguza akiongoza zoezi la kupanda malisho katika shamba la malisho la mifugo la Vikuge lililopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani. Zoezi hilo lilifanyika shambani hapo Aprili 19, 2023.
WADAU WAKUTANA KUJADILI UTAFITI KUONGEZA THAMANI SAMAKI AINA YA DAGAA.
Katibu Tawala mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa warsha ya kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya matokeo ya utafiti wa upotevu wa mazao ya uvuvi Nchini, April 19,2023 Mkoani Mwanza
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uvuvi Tanzania Bi. Flora Luhanga akiongea na wadau wa uvuvi (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwa ufunguzi wa warsha ya kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya matokeo ya utafiti wa upotevu wa mazao ya uvuvi Nchini Aprili 19, 2023 Mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) na mshauri mwelekezi wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), Bw. Yahya Mgawe (katikati) akitoa maelezo ya dagaa waliochakatwa na kufungashwa na wavuvi wadowadogo kwa Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana (wa pili kutoka kushoto) mara baada ya warsha ya kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya matokeo ya utafiti wa upotevu wa mazao ya uvuvi Nchini, April 19, 2023 Mkoani Mwanza.
Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Bw. Balandya Elikana (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya waliofanya utafiti wa upotevu wa mazao ya uvuvi nchini Tanzania Mara baada ya ufunguzi wa washra ya kupokea, kujadili na kupitisha taarifa ya matokeo ya utafiti wa upotevu wa mazao ya uvuvi Nchini, Aprili 19,2023 Mkoani Mwanza.