Nav bar

Alhamisi, 27 Aprili 2023

DKT. ASIMWE AONGOZA ZOEZI LA UPANDAJI WA MALISHO YA MIFUGO KATIKA SHAMBA LA VIKUGE. AELEZA MIPANGO YA SERIKALI YA KUTATUA CHANGAMOTO YA CHAKULA CHA MIFUGO NCHINI

 

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho na Rasilimali ya Vyakula vya Wanyama, Dkt. Asimwe Rwiguza (kulia) akikagua maendeleo ya Shamba Darasa  la malisho ya mifugo lililopo katika Kijiji cha Wami Sokoine, Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero, Mkoani Morogoro alipotembelea eneo hilo Aprili 19, 2023. kushoto ni  Mjumbe wa kikundi wa shamba darasa hilo, Bw. Jumbe Kamando. 

Wizara imeanzisha mashamba darasa 100 katika Halmashauri 44 nchini ili wafugaji waweze kujifunza kwa vitendo namna ya kuandaa, kupanda, kutunza na kuhifadhi malisho ya mifugo.

Mkurugenzi wa Idara ya Uendelezaji wa Maeneo ya Malisho na Rasilimali ya Vyakula vya Wanyama, Dkt. Asimwe Rwiguza akiongoza zoezi la kupanda malisho katika shamba la malisho la mifugo la Vikuge lililopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani. Zoezi hilo lilifanyika shambani hapo Aprili 19, 2023.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni